Wataalamu waonya matumizi ya limau kusafisha sehemu za siri ni hatari

October 5, 2020

Dakika 8 zilizopita

maji ya limau yana acid chungu nzima

Sehemu ya siri ya wanawake ni kiungo hatari sana ambacho kinahitaji kupewa uangalizi maalum.

Ni sehemu inayohitajika kusafishwa kwa umakini kwasababu magonjwa husambaa kwa haraka na kwa njia rahisi.

Wazazi na mababu zetu walikuwa wakisema vitu kama ndimu zinastahili kutumiwa kusafisha uke ili kuepusha harufu mbaya na magonjwa.

Hata hive kiutokana na sayansi, viungo maalum ambavyo havina madhara vimebuniwa ili kutumiwa kusafisha uke na mfumo wa uzazi, kwa mujibu wa Dk. Fatima Abdulahi, daktari bingwa wa wanawake katika hospitali ya kimataifa ya Marie Stopes mjini Abuja

Daktari fatima Abdullahi

Uhusiano kati ya ndimu na sehemu ya siri ya wanawake

Dk. Fatima anasema kuwa kisayansi kila kiungo katika mwili wa binadamu kina kemikali kama vile tindi kali na alkalini kwa kiwango kinachohitajika mwilini.

Kuwa na wingi wa kemikali hiyo kunaweza kuleta madhara japo kidogo.

“Maji ya limau yanasadikiwa kuwa na kiwango cha juu cha tindikali ambacho ni cha pili kwa ukubwa cha14/1/14, wakati uke wa mwanamke una kiwango cha kati ya a 3.8 / 14 na 4.5 / 14, cha tindikali” alisema.

Athari ya kutumia limau katika sehemu ya siri ya mwanamke

Kuna baadhi ya wanawake wanaodaiwa kutumia limau kujichua lakini wataalamu wanasema ni hatari kufanya hivyo kwsababu maji ya limau yana ukakasi wa hali ya juu ambao unabadilisha mfumo wa asilia ya uke.

Matumizi ya ndimu kusafisha uke kupita kiasi yanaweza kusababisha kusambaa kwa magonjwa katika eneo hilo, alisema daktari.

Utumizi wa limau kusafisha uke pia unaweza kuathiri shingo ya uzazi hali ambayo inaweza kusababisha saratani ya Shingo ya uzazi.

Majeraha yanayotokana na kuchibuka kwa sehemu za siri yanayotokana na matumizi ya limau wakati wa kujisafisha yanaweza kuchangia kusambaza virusi vya HIV.

Wanasayansi wamegundua kuwa sehemu za siri ni mahali wanawake wanapenda kusafisha mara kwa mara na japo ni vyema kufanya hivyo wanashauri uangalifu uzingatiwe wakati wa kufanya hivyo ili kujiepusha na maradhi.

Je kunywa maji ya limau kunaathiri wanawake kama inavyowaathiri wanaume?

Mwanamke akila limau

Daktari bingwa wa wanawake anasema kunywa maji ya limau hakuleti madhara kwa afya ya uzazi ya wanawake.

Zamani kuna baadhi ya watu walidai kwamba kunywa maji ya limau kwa wingi kunaweza kumfanya msichana kupoteza ubikira, lakini daktari anasema dhana hiyo haina msingi wowote wa kisayansi.

“Maji ya limau hukinga mwili dhidi ya magonjwa fulani, hutengeza ngozi iliyoharibika na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili na wakati mwingine hutumiwa kama chanzo cha Vitamin C,” alisema.

Ushauri wa jinsi ya kutumia limau

Limau linaweza kutumiwa kumaliza harufu mbaya mwilini kwa jinsia zote

Lakini unashauriwa usitumie maji ya limau pekee, badala yake changanya na maji kuvunja makali yake ili kujiepusha na maabukizi ya magonjwa kama nilivyotaja hapo awali. Anasema Dk Fatima.

Dk. Fatima anasema utafiti uliofanywa barani Ulaya kuhusu matumizi ya limau, unaonesha kuwa wanawake wanaotumia maji ya limau pekee kusafisha sehemu zao za siri wanakabiliwa na hatari ya kupatikana na magonjwa tofauti.

Wakati wa kusafisha sehemu za siri wanawake wanashauriwa kutumia maji ya vugu vugu kwa uangalifu kwasababu yakiwa moto zaidi pia maji hayo yanaweza kusababisha magonjwa mengine.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *