Washukiwa watatu wa mauaji ya kimbari Rwanda wakamatwa Ubelgiji,

October 4, 2020

 

Watu watatu wanaoshukiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari ya Rwanda 1994 wamekamatwa na kushtakiwa nchini Ubelgiji kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, ofisi ya mwendesha mashtaka imesema jana Jumamosi. 

Ofisi hiyo haikutoa maelezo juu ya watu hao lakini imesema waliweza kutambuliwa kwa msaada wa maelezo ya mashuhuda wa nchini Rwanda katika uchunguzi uliofanywa na Ubelgiji. 

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Rwanda baadaye iliwataja watatu hao kuwa ni Pierre Basabose, Seraphin Twahirwa na Christophe Ndangali na kutoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwao. 

Mauaji ya kimbari ya 1994 yalipoteza maisha ya watu 800,000, wengi wao wakiwa Watutsi lakini pia Wahutu wenye msimamo wa wastani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *