Wapinzani wa Brexit waandamana Brussels,

October 16, 2020

 

Wananchi wanaopinga mchakato wa Brexit unaotaka Uingereza ijiondoe Jumuiya ya Ulaya (EU), walifanya maandamano katika mji mkuu wa Brussels nchini Ubelgiji.

Waandamanaji hao walikusanyika karibu na eneo linaloandaliwa mkutano wa baraza la EU mjini Brussels, na kupinga mchakato wa Brexit huku wakiitaka Uingereza isijitenge na jumuiya.

Waandamanaji hao walibeba mabango yenye maandishi yanayopinga Brexit, na baadaye kuyaacha chini.

Baadaye waandamanaji hao wakasoma taarifa za waandishi wa habari, kisha wakatawanyika huku wakitoa kelele za kaulimbiu yao.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *