Wapiganaji wa Kiislamu waviteka visiwa vingine 2 Msumbiji, on September 13, 2020 at 3:00 pm

September 13, 2020

Wanajihad kaskazini mwa Msumbiji waliviteka visiwa viwili vidogo vya bahari hindi na kutishia usafiri wa baharini katika eneo hilo ambapo mradi wa gesi yenye thamani ya mabilioni ya madola unajengwa kulingana na wakaazi.Hatua hiyo ndio ya hivi karibuni katika mkoa huo wa Cabo Delgado katika kipindi cha miaka mitatu iliopita.Inajiri mwezi mmoja baada ya Wanajihad hao wanaohusishwa na kundi la Islamic State kuteka mji wa bandari ya kimkakati ya Mocimboa da Pria, ambayo ilitumika kusafirisha mizigo ya ujensi wa mradi huo wa gesi.Mashahidi waliambia chombo cha habari cha AFP kwamba wapiganaji hao waliteka kisiwa cha Mecungo na Vamisse siku ya Jumatano usiku.”Waliwasili usiku wakiwa katika boti ndogo ya kuvulia samaki . walitoa watu katika nyumba zao na kuzichoma”, alisema mkaazi mmoja ambaye alikuwa ametoroka katika kisiwa cha Mocimboa da Pria.”Hawakumdhuru yeyote , walitoa maagizo ya watu kuondoka katika kisiwa hicho”, alisema kwa njia ya simu , akiongezea kwamba ameelekea ndani zaidi ya mji huo wa madini wa Montepuez baada ya kuvuka hadi kisiwani humo kwa kutumia boti na baadaye kusafiri kwa basi hadi Montepuez.Visiwa hivyo vilikuwa vikiishi watu waliopoteza makaazi yao waliotoroka vijiji vya eneo la bara ambalo mashambulizi yameongezeka.Shahidi mwengine anasema kwamba kabla ya nyumba hizo kuchomwa , Wanajihad hao walifanya mkutano na wakaazi na kuwaagiza kuondoka katika kijiji hicho.”Walitukusanya pamoja na kutuambia kutoroka iwapo tunataka kuishi. Nadhani kila mtu aliondoka katika kisiwa hicho” , mtu mmoja ambaye hakutaka kutambulika alisema.Wapiganaji hao wamekuwa wakitekeleza mashambulio tangu 2017, na kuwawacha watu 250,000 bila makao huku wakiwaua watu 1500.Vikosi vya serikali bado vinakabiliana na wapiganaji hao ili kuikomboa bandari ya Mocimboa da Pria tangu Agosti 12.Mashambulio ya wapiganaji hao katika Cabo Delgado yamesababisha uharibifu mkubwa wa barabara kati ya mji mkuu wa mkoa huo Pemba na eneo lenye utajiri wa gesi la Palma kutopitika.Usafiri wa baharini ndio uliokuwa umesalia kwa mizigo kupita.Lakini kampuni ya mafuta ya Ufaransa Total , ambayo inawekeza dola bilioni 23 katika mradi wa uchimbaji wa gesi ilisema kwamba haitegemei tena bandari ya Mocimboa da Praia kama eneo la kimkakati na kwamba sasa imejenga vifaa vyake baharini , Total ilisema katika barua pepe ya maswali.Maafisa wa polisi katika eneo hilo wamekataa kuzungumzia kuhusu kutekwa kwa kisiwa hicho.,

Wanajihad kaskazini mwa Msumbiji waliviteka visiwa viwili vidogo vya bahari hindi na kutishia usafiri wa baharini katika eneo hilo ambapo mradi wa gesi yenye thamani ya mabilioni ya madola unajengwa kulingana na wakaazi.

Hatua hiyo ndio ya hivi karibuni katika mkoa huo wa Cabo Delgado katika kipindi cha miaka mitatu iliopita.

Inajiri mwezi mmoja baada ya Wanajihad hao wanaohusishwa na kundi la Islamic State kuteka mji wa bandari ya kimkakati ya Mocimboa da Pria, ambayo ilitumika kusafirisha mizigo ya ujensi wa mradi huo wa gesi.

Mashahidi waliambia chombo cha habari cha AFP kwamba wapiganaji hao waliteka kisiwa cha Mecungo na Vamisse siku ya Jumatano usiku.

”Waliwasili usiku wakiwa katika boti ndogo ya kuvulia samaki . walitoa watu katika nyumba zao na kuzichoma”, alisema mkaazi mmoja ambaye alikuwa ametoroka katika kisiwa cha Mocimboa da Pria.

”Hawakumdhuru yeyote , walitoa maagizo ya watu kuondoka katika kisiwa hicho”, alisema kwa njia ya simu , akiongezea kwamba ameelekea ndani zaidi ya mji huo wa madini wa Montepuez baada ya kuvuka hadi kisiwani humo kwa kutumia boti na baadaye kusafiri kwa basi hadi Montepuez.

Visiwa hivyo vilikuwa vikiishi watu waliopoteza makaazi yao waliotoroka vijiji vya eneo la bara ambalo mashambulizi yameongezeka.

Shahidi mwengine anasema kwamba kabla ya nyumba hizo kuchomwa , Wanajihad hao walifanya mkutano na wakaazi na kuwaagiza kuondoka katika kijiji hicho.

”Walitukusanya pamoja na kutuambia kutoroka iwapo tunataka kuishi. Nadhani kila mtu aliondoka katika kisiwa hicho” , mtu mmoja ambaye hakutaka kutambulika alisema.

Wapiganaji hao wamekuwa wakitekeleza mashambulio tangu 2017, na kuwawacha watu 250,000 bila makao huku wakiwaua watu 1500.

Vikosi vya serikali bado vinakabiliana na wapiganaji hao ili kuikomboa bandari ya Mocimboa da Pria tangu Agosti 12.

Mashambulio ya wapiganaji hao katika Cabo Delgado yamesababisha uharibifu mkubwa wa barabara kati ya mji mkuu wa mkoa huo Pemba na eneo lenye utajiri wa gesi la Palma kutopitika.

Usafiri wa baharini ndio uliokuwa umesalia kwa mizigo kupita.

Lakini kampuni ya mafuta ya Ufaransa Total , ambayo inawekeza dola bilioni 23 katika mradi wa uchimbaji wa gesi ilisema kwamba haitegemei tena bandari ya Mocimboa da Praia kama eneo la kimkakati na kwamba sasa imejenga vifaa vyake baharini , Total ilisema katika barua pepe ya maswali.

Maafisa wa polisi katika eneo hilo wamekataa kuzungumzia kuhusu kutekwa kwa kisiwa hicho.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *