Wanyamapori walioungua kwa moto watibiwa kwa ngozi ya samaki

October 19, 2020

Dakika 6 zilizopita

Anteater paw wrapped in tilapia skin

Onyo tarifa hii ina picha za kuogofya za wanyama waliojeruhiwa

Ni kama kiumbe kinachoonekana katika sinema : Kiumbe chenye umbo kubwa cha rangi ya kahawia , chenye nywele zilizofunika mwili wake …ngozi ya samaki.

Lakini kilichofanyika ni ufundi tu ambao umekuwa ukitumiwa kusaidia kupona haraka kwa wanyama waliojipata katika moto mbaya zaidi wa nyikani uliolikumba eneo la Pantal, ambalo ni eneo kubwa zaidi duniani lenye uoto wa kitropiki kuwahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa.

Moto huo umeteketeza 27% ya eneo hilo, ambalo ni moja wapo ya maeneo yenye bayoanuwai zaidi duniani, eneo hilo likianzia Brazil na kuingia katika mataifa jirani ya Bolivia na Paraguay.

Pantanal pia ni eneo lenye wingi wa viumbe wengi wa jamii ya mamalia duniani , wakiwemo chui – ambao wameathiriwa vibaya na moto.

Tiba ya ngozi ya samaki.

Vets operate on a tapir cub burned during the Pantanal fires

Maelezo ya picha,

Jeraha la mkono wa wa tapir limefungwa ili kumzuwia kupoteza maji na damu na kutunza kidonda

Ngozi ya Sato , kutoka maji baridi, imekuwa ikitumika kutibu vidonda vya tapir wawili wachanga na a nyoka aina ya chatu.

Anayefuatia ni ndege wa jamii ya bata mzinga- ambao ni kama utambulisho wa eneo la Pantanal.

“Ngozi ya Sato ina kiwango kikubwa cha ‘collagen’, ambayo ina nafasi kubwa katika mchakato wa kuponya vidonda vinavyosababishwa na kuungua ,” anasema Felipe Rocha,mtafiti katika Chuo Kikuu cha Ceara (UFC), ambako mbinu hii iligunduliwa.

Ngozi za samaki zinaletwa na wafugaji wa samaki .

Ngozi hizo zinakaushwa , kunyunyiziwa dawa ya kuua vijidudu na kutunzwa nadi ya chumba chenye joto la kawaida.

Zinatumiwa kama vifuniko vya kibaiolojia vya majeraha, na kusaidia mchakato wa kupona.

Mlipuko wa bandari ya Beirut

Fish skin with researchers in the background

Maelezo ya picha,

Watafiti wamekuwa wakitumia mbinu hii kutibu majeraha ya watu walioungua katika hospitali tangu mwaka 2015

Watafiti wamekuwa wakitumia mbinu hii kutibu majeraha ya watu walioungua katika hospitali tangu mwaka 2015

Mwezi Agosti, Chuo kikuu kilituma sentimita 40,000 za mraba za ngozi ya samaki kwa ajili ya kutibu vidonda baada ya mlipuko wa bandari ya Beirut , uliowauwa watu 203 na kuwajeruhi maelfu kadhaa.

Wamekuwa wakishirikiana na watafiti wa Chuo kikuu cha Davis kusaidia kuwatibu duma waliojeruhiwa katika mioto iliyowaka California mwaka 2018.

Rocha na wenzake walihisi kuwa kusikitishwa na picha za kusikitisha za wanyama wa nyikani waliokuwa na majeraha ya kuungua kwa moto ulioanza katika Pantanal.

Kwa kuwasiliana na shirika lisilo la kiserikali(NGO) la wanyamapori Ampara, aliwasiliana na madaktari wa mifugo katika chuo Kikuu cha kitaifa cha Mato Grosso kilichopo Cuiaba, ambako kwa saa wanashirikisha wahudumu ujuzi wao huo wa kutibu majeraha ya moto ya wanyama kwa kutumia ngozi ya samaki

Rocha anasema kuwaona wanyama wakipona ‘inamfariji saana’.

Maumivu kidogo na kupoteza majimaji

An adult female jaguar with burnt paws receives treatment

Maelezo ya picha,

Wahifadhi wa mazingira wanahofu juu ya athari za wanyama pori za moto mkubwa kuwahi kushuhudia kwa miongo kadhaa latika Pantanal

Kwa kawaida, mafuta yangepakwa kwenye vidonda vyao na bandeji ingewekwa na kubadilishwa kila siku

“Kwa kutumia ngozi ya tilapia , tunapunguza ya garama kubadilisha bandeji kila siku, tunapunguza maumivu kwa myama na kupunguzia kazi wahudumu wanaowahudumia wanyama ,” Rocha anasema.

Ngozi ya samaki inakazwa vizuri na kufunika kidonda na kukifanya kiendelee kuwa na joto na hivyo kuwazuwia wadudu kukivamia.

Na ngozi ya mnyama hurejea katika muonekano wake wa awali.

An adult tapir has had patches of tilapia skin on its back

Maelezo ya picha,

Ngozi ya Tapir aliyekuwa ameumia amerejea kuwa na ngozi yake ya kawaida baada ya kidonda chake kufunikwa kwa ngozi ya samaki

Kalungu aliyeungua kwenye miguu yake yote minne alikuwa ni mnyama wa kwanza kuwekewa ngozi ya samaki . Halafu Tapir wengine wawili wakubwa na mmoja mchanga wakapewa huduma.

Aliyefuatia alikuwa ni nyoka aina ya chatu , ambaye ngozi yake iliungua sana hadi ndani nyama yake ilikuwa inaonekana.

Felipe Rocha treating an anaconda snake

Rocha anasema wanyama wapo kwenye maumivu makali.

“Tunafurahi kuwa tunaweza kuwasaidia katika wakati mgumu kama huu nchini humu,”aliongeza.

Pantanal imekuwa na jangwa kubwa kwa miaka sita , jambo ambalo lilisababisha moto kushika kasi, taarifa rasmi za takwimu zinasema.

Wataalamu wanasema oto huo umesababishwa na shughuli za binadamu.Makundi ya mazingira yamemkosoa rais Jair Bolsonaro kwa kushindwa kukabiliana na moto huo mapema.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *