Wangambo 10 na raia 5 wauawa katika ghasia Mashariki mwa Congo, noreply@blogger.com (Muungwana Blog), on August 30, 2020 at 5:00 pm

August 30, 2020

Jeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limesema kuwa wanamgambo 10 wa kundi linalojiita dola la kiislamu, IS waliuawa baada ya kuvamia msafara wa wanajeshi katika eneo la Mashariki mwa Congo siku ya Ijumaa huku kiongozi mmoja wa kijamii akisema kuwa raia watano waliuawa baadaye na wanachama wa kundi hilo la waasi.Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, kikundi cha wanamgambo cha Allied Democratic Forces ADF ambacho kimekuwa kikifanya shughuli zake Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa muda wa miongo mitatu iliyopita, kimewauwa zaidi ya raia elfu 1 tangu mwanzoni mwa mwaka 2019.Hali hiyo ya ukosefu wa usalama imewalazimisha maelfu ya raia nchini humo kukimbia makazi yao na kutatiza harakati za Congo za kukabiliana na janga la virusi vya corona pamoja na janga la ugonjwa wa Ebola ambalo limesababisha zaidi ya vifo vya watu 2200.,

Jeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limesema kuwa wanamgambo 10 wa kundi linalojiita dola la kiislamu, IS waliuawa baada ya kuvamia msafara wa wanajeshi katika eneo la Mashariki mwa Congo siku ya Ijumaa huku kiongozi mmoja wa kijamii akisema kuwa raia watano waliuawa baadaye na wanachama wa kundi hilo la waasi.

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, kikundi cha wanamgambo cha Allied Democratic Forces ADF ambacho kimekuwa kikifanya shughuli zake Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa muda wa miongo mitatu iliyopita, kimewauwa zaidi ya raia elfu 1 tangu mwanzoni mwa mwaka 2019.

Hali hiyo ya ukosefu wa usalama imewalazimisha maelfu ya raia nchini humo kukimbia makazi yao na kutatiza harakati za Congo za kukabiliana na janga la virusi vya corona pamoja na janga la ugonjwa wa Ebola ambalo limesababisha zaidi ya vifo vya watu 2200.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *