Wanawake wakemea vitendo vya udhalilishwaji,

October 14, 2020

 

Na Timothy Itembe Mara.

WANAWAKE wamekemea vitendo  wanavyofanyiwa vya udhalilishwaji na baadhi ya watu wakiwatukana wanawake wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi.

Akiongea mgombea ubunge viti maalumu kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA),Tekra Johanes kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi zinazoendelea ili kufikia uchaguzi wa mwaka 20202alisema kuwa kitendo cha mwanamke mgombea kudhalilishwa ni kitendo cha kulaaniwa na kukemewa

Tekra aliongeza kuwa katika mikutano ya kampeni za uchaguzi inayoendelea mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini,Esther Matiko amekuwa akidhalilishwa na baadhi ya watu huku wengine wakiwa ni viongozi kama vile Askari polisi moja alie mtukana juzi wakati akitoka kwenye kampeni za uchaguzi.

“Kama ningemjua mmoja wa Askari polisi aliye mtukana mgombea wangu tena askari huyo wa kiume bila aibu alimtolea matusi ya nguoni mgombea wangu wa ubunge jimbo la Tarime,Esther Matiko ningemfahamu jina lake ningelihamasisha wakina mama kuchukua hatua za kuandamana hadi kwa IGP Saimoni Sillo ili kumsema na kumshitaki kwa lengo la kuchukuliwa hatua na kupinga kitendo hicho”alisema Tekra.   

Mwanamama huyo alimaliza kwa kusema kuwa licha ya kuwa mwanamke kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ni moja ya kikatiba ambapo kugombeani haki ya kila mtu lakini bado kuna baadhi ya watu wenye fikra mgando wanatumia mawazo hayo kuwadhalilisha wanawake wagombea  jambo hilo hatutakubali tutalipinga hadi kwenye ngazi zinazohusika.

Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini kupitia (CHADEMA),Esther Matiko alisema kuwa ataenda kumsinda mpinzani wake wa Chama cha mapinduzi (CCM) Michael Kembaki kwa kura nyingi ambazo hataamini.

Matimo aliongeza kusema kuwa wakati akiwa mbunge ameleta maendeleo ndani ya jimbo la Tarime tofauti na watangulizi wake ambapo alitolea mfano wa shule ya sekondari Rebu kuwa alipeleka mabati 225 wakati akiwa gerezani.

Matiko alimaliza kwa kusema kuwa licha ya kuwa wanambeza na kumtukana kwenye majukwaa amejenga historia ndani ya mji wa Tarime,Tanzania na ulimwengu mzaima wakati aliposhinda kiti cha ubunge mwaka 2015 na kuingia bungeni na kuvunja mila kandamizi zilizokuwepo kuwa mwanamke hawezi kugombea na kuwa kingozi na kuwa hiyo amewaletea wanawake sifa na amewafungulia mlango.

Chacha Mwita maarufu Pamba alisema kuwa kampeni za uchaguzi ni raha na kila moja anatakiwa kuinjoi na kunadi sera za chama chake cha kuwa nini ataenda kuwafanyia wananchi pindi watakapoingia madarakani siovinginevyo.

Bashiri Selemani maarufu (SAUTI) aliomba Tume ya Taifa ya uchaguzi kusimamia uchaguzi na kuwa wa uhuru na haki ili atakae shinda kupitia wananchi kumwamini na kumchaghua atanagazwe siovinginevyo.

Sauti ambae pia ni mgombea udiwani kata ya Nyamisangura kupitia tiketi ya CHADEMA aliongeza kuwa Amani iliyopo ipo mikononi mwa wananchi na asitokee mtu moja anajaribu kuvuruga amani hiyo kwa masilahi yake binafsi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *