Wanawake elfu 10 waandamana kumtaka rais wa Belarus kujiuzulu, on September 13, 2020 at 7:00 am

September 13, 2020

 Takriban wanawake elfu 10 walifanya maandamano ya kelele katika mji mkuu wa Belarus, Minsk hapo jana wakitaka kujiuzulu kwa rais wa nchi hiyo Alexander Lukashenko katika siku ya 35 ya mfululizo wa maandamano makubwa dhidi ya serikali ya nchi hiyo. Waandamanaji wengi walibeba picha za Maria Kolesnikova, kiongozi wa baraza la uratibu la upinzani linalotaka kuandaliwa kwa uchaguzi mpya wa urais katika taifa hilo lililokuwa la muungano wa kisovieti, aliyefungwa gerezani wiki hii baada ya polisi kujaribu kumfurusha kwa lazima kutoka nchini humo. Waandamanaji wengine walibeba mabango yaliokuwa yameandikwa ”ulipaka moyo wangu na machungu ya samawati” wakimaanisha madai ya Lukashenko kwamba awali baadhi ya wanawake walijipaka rangi kuonyesha kuwa walipata majeraha baada ya kupigwa na polisi. Kundi la kutetea haki za binadamu la Viasna, limesema kuwa zaidi ya watu 70 walikamatwa wakati wa maandamano hayo. Lukashenko amekataa kukutana na baraza hilo na viongozi wengi wamezuiliwa ama kuondoka nchini humo.,

 

Takriban wanawake elfu 10 walifanya maandamano ya kelele katika mji mkuu wa Belarus, Minsk hapo jana wakitaka kujiuzulu kwa rais wa nchi hiyo Alexander Lukashenko katika siku ya 35 ya mfululizo wa maandamano makubwa dhidi ya serikali ya nchi hiyo. 

Waandamanaji wengi walibeba picha za Maria Kolesnikova, kiongozi wa baraza la uratibu la upinzani linalotaka kuandaliwa kwa uchaguzi mpya wa urais katika taifa hilo lililokuwa la muungano wa kisovieti, aliyefungwa gerezani wiki hii baada ya polisi kujaribu kumfurusha kwa lazima kutoka nchini humo. 

Waandamanaji wengine walibeba mabango yaliokuwa yameandikwa ”ulipaka moyo wangu na machungu ya samawati” wakimaanisha madai ya Lukashenko kwamba awali baadhi ya wanawake walijipaka rangi kuonyesha kuwa walipata majeraha baada ya kupigwa na polisi. 

Kundi la kutetea haki za binadamu la Viasna, limesema kuwa zaidi ya watu 70 walikamatwa wakati wa maandamano hayo. 

Lukashenko amekataa kukutana na baraza hilo na viongozi wengi wamezuiliwa ama kuondoka nchini humo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *