Wanasayansi wafanyia utafiti kitakachoangamiza dunia na jinsi ya kuokoa ulimwengu

October 13, 2020

Dakika 10 zilizopita

Dunia ikiangamia

Dunia imeishi kwa takriban karne milioni 45 na hivi sasa tunashuhudia historia ya kipekee.

“Ni karne ya kwanza ambayo viumbe, wetu, walikua na nguvu kubwa na iliyokuwa ikitawala kiasi cha mustakabali wa dunia kuwa mikononi mwake “, anaandika mnajibu wa Kiingereza Martin Rees katika andiko lake la “in the future. Prospects for humanity “.

“Kilichopo sasa ni muhimu zaidi kuliko kinachotokea katika karne hii kitakuwa na athari kwa maelfu ya miaka, ” anasema katika kitabu chake cha mwaka 2018.

Reese kwa kweli amekuwa akirudia tahadhari hizi kwa zaidi ya miongo miwili, ambayo kwa watu wengi ni jambo zuri, lakini pengine kwa wakati ule, zaidi ya sayansi, yalionekana kama sayansi ya kufikirika.

Hakika, yeye mwenyewe alitambua hilo kwenye mazungumzo ya kipindi cha TED ” tunahofia kupita kiasi kuhusu hatari ndogo ndogo; ajali ya ndege isiyo yumkinika , vyakula vinavyoweza kusababisha saratani , dozi ndogo ya mionzi…. lakini sisi na wanasiasa wanaotuongoza wanaishi katika kuukataa ukweli wa hali ilivyo. Majanga”.

Kisha mwaka 2020 ukaja na kila neno litokalo kwa bwana Rees ni ukweli wa kuogofya.

Vifo milioni moja kutokana na virusi vya corona: takwimu zinazoonesha ni miji gani iliyokumbwa kwa kiasi kikubwa na janga hilo Kwa mfano, kwenye mazungumzo aliyoyatoa mwaka 2014, alisema hivi sasa “hatari mbaya inatoka kwetu wenyewe”: Na si tu kuna tishio la nyukilia.

Katika dunia yetu … usafiri wa anga unaweza kusababisha kusambaza majanga kwa siku kadhaa, na mitandao ya kijamii inaweza kusambaza na kupandikiza hali ya uoga na tetesi kwa haraka mithili ya mwanga unavyosafiri.”

Hatahivyo, kuna wale ambao hawakuhitaji ugonjwa wa Covid -19 kumsikiliza Reese. Tangu mwaka 2015 kundi dogo la watafiti walikuwa wakifanya kazi chini ya uangalizi wake katika kituo cha stadi za hatari zilizopo (CSER) katika Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza.

Kituo , ambacho kilizingatia ushauri wa viongozi kutoka kwa wasomi-Kama vile mwanafizikia Stephen Hawking-na kutoka katika maeneo mengine kama nafanyabiashara Elon Musk-kilitafiti hatari inayoweza kusababisha kutoweka kwa ubinadamu na namna gani hali hiyo inaweza kupunguzwa.

Mwanabaiolojia Clarissa Rios Rojas, alijiunga na kituo cha CSER mwezi Machi, muda mfupi kabla serikali ya Uingereza kabla Haijatoa tangazo la karantani.

CLARISSA RÍOS ROJAS

“Tumekuwa na majanga kabla na bado Covid-19 nayo imetukamata,”

Rios aliiambia BBC idhaa ya Mundo.

“Hivyo makosa yalitokea wapi? Tunaweza kujifunza nini kutokana na majaribio na jinsi gani tunaweza kujiandaa tena siku za usoni”?

Kwa maneno mengine, kazi yake katika chuo cha Cambridge ni kubaini kwa nini utabiri unaotokana na data za kisayansi hausikilizwi, ili kusaidia kutengeneza sera za Umma ambazo huandaa binadamu kwa ajili ya janga la dunia litakalofuata.

Kama ilivyo kwa athari mbaya zilizotokana na virusi vya corona ,virusi hivyo si kitu cha kwanza na wala cha mwisho.

Maeneo matano hatari

Kitu cha kwanza ambacho Rios anaeleza ni kuwa kuna tofauti kati ya janga na hatari iliyopo.

Ingawa maana yake zinafanana kwa namna fulani kati ya hayo, kwa ujumla inaeleweka kuwa matukio ya hatari ya kuwa majanga, ni kuwa ikiwa yatatokea yataua 10% ya watu duniani au kusababisha uharibifu kama huo.

Kwa mfano tukio la karibuni , inaelezwa kuwa tukio baya la karne ya 20 ilikua janga la mafua la mwaka 1918, lililofahamika kama mafua ya Uhispania, ambapo asilimia moja na tano ya watu duniani walipoteza maisha.

Kitu cha kwanza ambacho Rios anaeleza ni kuwa kuna tofauti kati ya janga na hatari iliyopo.

CSER imetafiti matukio aina tofauti, ambayo yamegawanywa katika maeneo matano makubwa: kibaiolojia, kimazingira, hatari za kiteknolojia, zinazotokana na intelijensia bandia na hali ya kutokuwepo kwa usawa.

Baadhi ya mifano iko wazi kabisa kama vile majanga katika mazingira ya kibaiolojia au mabadiliko ya tabia nchi .

Lakini kuna hatari nyingine zilizopo kama intelijensia bandia.

“Hofu ya intelijensia bandia si kama ile ya kufikiria kuwa Anorld Schwarzenegger ataibuka na kutuua sote,” anasema Rios akirejelea filamu ya Terminator.

“Kiuhalisia hutokea kwamba kufikia malengo ya kumuokoa mwanadamu, mfumo wote wa ikolojia unaharibiwa kwasababu hakuna mipaka muhimu iliyotolewa kuongoza intelijensia hiyo,” anaeleza.

Martin Rees ni mmoja ya watafiti wakubwa duniani

Katika hili, kazi ya Rio itakuwa kwa mfano , kufanya kazi pamoja na serikali kutengeneza protokali na kuzifuatilia zana kwa ajili ya taasisi katika maeneo husika, au kuhakikisha kuwa programu za utafiti za vyuo vikuu vinavyo husika na uhandisi vina misingi imara ya maarifa na maadili.

Hatari ya kutokuwepo kwa usawa ni eneo jingine ambalo hatari yake haiwezi kubainika lakini kuna mfano wa wazi mdogo sana katika historia;

Ukosefu wa haki za kijamii ni eneo lingine ambalo kiwango chake cha hatari hakiwezi kuonekana. Lakini kuna mfano wazi kabisa katika historia: Ushindi wa Ulaya kwa Amerika.

Tukio hilo ” lilisababisha kupotea kwa asilimia 80 ya jamii ndogo , kuanguka kwa Aztec, Inca na Zapotec, vifo na mateso, kuharibiwa kwa tamaduni na kuyumba kisiasa kulikotokea kama matokeo ya biashara ya utumwa baina ya mabara ” CSER imeeleza katika tovuti yake.

Viruis vya corona vimeonesha jinsi mifumo inavyoweza kuanguka moja baada ya mwengine

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *