Wanaongeza uzito kwenye kororsho kwa kutumia kokoto kukiona, on September 12, 2020 at 1:00 pm

September 12, 2020

Na Faruku Ngonyani , Mtwara.Kuelekea msimu mpya wa zao la kororsho 2020/21, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya ametoa onyo  kwa atakaebainika na kosa la kuongeza uzito kwa kokoto atachukuliwa hatua kali za kisheria.Kauli hiyo ameitoa akiwa kwenye kikao kilichowajumuisha viongzo wa vyama 67 vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) vilivyopo katika Halmashauri 3 zilizopo Wilaya ya Mtwara.‘‘nitoe wito kwa mtu yeyote akayejihusisha na tabaia hiyo ya kuongeza kilo za korosho kwa kuongeza kokoto atashughulikiwa vizuri tu na sipo tayari kuona zao hili linapotza ubora wake’’Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa kwa sasa ni vyema Viongozi wa vyama vya msingi vya Ushirika  (AMCOS) kutengeza mahusiano mazuri na viongozi wa Halmashauri ili kuweza kuboresha za o hilo kwa msimu wa 2020/21.Aidha Mkuu wa Wilaya ametumia fursa hiyo kwa kusikiliza kero na changamoto  zinazowakabili  viongozi hao  ambapo viongozi hao wameelezea zao ikiwa ni pamoja na madai yao ya pesa ya ushuru ya msimu mwa mwaka 2019/2020.Changamoto zingine ikiwa ni pamoja na  kucheleweshwa kwa fedha za wakulima ,kupotea kwa ubora wa korosho na ukosefu wa  mahusiano mazuri kati ya Amcos na viongzi wa Halmashuri.Kwa upande wa viongozi hao wa vyma vy msingi vya Ushirika  wamesema kuwa na ni vyema kwaa Serikali wakawapeleka wataalam wenye weledi juu ya zao hilo la korosho  lakini   pia kushughulikia changamaoto ya vifungashio vya zao hilo la korosho kwa msimu huu mpya wa 2020/21.,

Na Faruku Ngonyani , Mtwara.

Kuelekea msimu mpya wa zao la kororsho 2020/21, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya ametoa onyo  kwa atakaebainika na kosa la kuongeza uzito kwa kokoto atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kauli hiyo ameitoa akiwa kwenye kikao kilichowajumuisha viongzo wa vyama 67 vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) vilivyopo katika Halmashauri 3 zilizopo Wilaya ya Mtwara.

‘‘nitoe wito kwa mtu yeyote akayejihusisha na tabaia hiyo ya kuongeza kilo za korosho kwa kuongeza kokoto atashughulikiwa vizuri tu na sipo tayari kuona zao hili linapotza ubora wake’’

Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa kwa sasa ni vyema Viongozi wa vyama vya msingi vya Ushirika  (AMCOS) kutengeza mahusiano mazuri na viongozi wa Halmashauri ili kuweza kuboresha za o hilo kwa msimu wa 2020/21.

Aidha Mkuu wa Wilaya ametumia fursa hiyo kwa kusikiliza kero na changamoto  zinazowakabili  viongozi hao  ambapo viongozi hao wameelezea zao ikiwa ni pamoja na madai yao ya pesa ya ushuru ya msimu mwa mwaka 2019/2020.

Changamoto zingine ikiwa ni pamoja na  kucheleweshwa kwa fedha za wakulima ,kupotea kwa ubora wa korosho na ukosefu wa  mahusiano mazuri kati ya Amcos na viongzi wa Halmashuri.

Kwa upande wa viongozi hao wa vyma vy msingi vya Ushirika  wamesema kuwa na ni vyema kwaa Serikali wakawapeleka wataalam wenye weledi juu ya zao hilo la korosho  lakini   pia kushughulikia changamaoto ya vifungashio vya zao hilo la korosho kwa msimu huu mpya wa 2020/21.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *