Wanamgambo na ‘laana’ ya utajiri wa gesi na madini ya rubi Msumbiji

September 18, 2020

Dakika 3 zilizopita

Mwanaume wa kiislamu akisali nchini Msumbiji

Jeshi la Msumbiji linashindwa kuukomboa mji wa bandari kutoka wanamgambo wa kiislamu (IS), mji huo ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza hifadhi kubwa ya gesi asilia barani Afrika-Kwa miaka mitatu taifa hilo limevamiwa na waasi na kufanya rasilimali hiyo kuwa laana nyingine katika nchi hiyo, anaandika mchambuzi wa Msumbiji Joseph Hanlon.

Hatimaye rais Filipe Nyusi anakabiliwa na uhalisia wa laana ya rasilimali.

Waasi wanaajiri wanachama wengine zaidi kwa kutumia udhaifu wa umasikini wa vijana Kaskazini mwa Msumbiji, alieleza katika hotuba yake hivi karibuni huko Pemba, mji mkuu mkuu wa Cabo Delgado.

Na alikiri kuwa licha ya kuwa majimbo matatu ya kaskazini – Cabo Delgado, Niassa na Nampula – wana utajiri mzuri wa asilia na uwezo mkubwa katika kilimo, lakini wako katika kiwango cha juu cha umaskini.

Mocimboa da Praia limedhibitiwa na wanamgambo tangu kati kati ya mwezi Agosti

Kwa miaka 15, kipato cha ndani cha Msumbiji kiliongezeka kwa asilimia sita 6% kwa mwaka, ongezeko hilo likitokana na rasilimali asilia kama makaa ya mawe, utengenezwaji wa umeme wa nguvu ya maji,kemikali ya atomiki na rasilimali nyingine.

Ingawa bado wananchi wengi wakiwa hawajafanikiwa na rasimili hizo, umasikini na kutokuwa na usawa vyote viliongezeka.

Kugundulika kwa amana kubwa ya rubi na eneo kubwa la kuchimba gesi nyingi ya asilia huko Cabo Delgado mwaka 2009-10, kulileta matumaini ya ajira na maisha bora kwa wananchi wengi lakini matumani hayo yalipotea ghafla.

Ilidaiwa kuwa faida ilikuwa inachukulitwa na kundi la wachache katika chama cha Frelimo ambacho kimetawala Msumbiji tangu taifa hilo lipate uhuru mwaka 1975.

Chanzo cha kukua kwa uasi wa kundi la kiislamu

Vita iliyoanza Oktoba 05, mwaka 2017 wakati kundi la waasi walipoteka miji na bandari ya Mocimboa da Praia kwa muda wa siku mbili.

Mji huo ulikuwa kilomita 60 kama maili 32 kusini kutoka katika mji wenye eneo kubwa la maendeleo ya gesi huko Palma na bandari ni muhimu kwa ajili ya mradi wa gesi kwa ajili ya kuisambaza.

Uasi huo uligunduliwa na wakazi wa eneo hilo.

Tangu wakati huo, vita iliongezeka na watu wapatao 1,500 waliuawa na wengine wapatao 250,000 walikimbia makazi yao.

Maelfu wamekimbia makazi yao na kupoteza vyanzo vyao vya mapato miezi michache iliyopita

Mji wa Cabo Delgado una waislamu wengi na kuna muhubiri mpya, wote wakiwa ni kutoka Afrika Mashariki na Msumbiji walipata malipata mafunzo kutoka ughaibuni, walianzisha misikiti na kudai kuwa maimamu wa mji huo walikuwa washirika wa Frelimo na walishiriki kuwanyang’anya utajiri wao.

Baadhi ya misikiti hii mipya inatoa fedha kwa ajili ya kusaidia wananchi kuanzisha biashara na kutoa mianya ya ajira – na waislamu walidai kuwa jamii ya waisalmu itakuwa vizuri chini ya uongozi wa Sharia.

Sasa rais Nyusi amekiri kuwa kuwa walivutiwa.

Kurejea kwa vita vya kupambana na ukoloni

Kulikuwa na makabiliano ya ghasia mwaka 2015 kati ya polisi na viongozi wa kimila wa kiislamu wakati walipojaribu kuzuia mafunzo ya wanamgambo wa kiislamu ambayo yalisababisha shambulio la kwanza kutokea Mocimboa da Praia.

Kiuhalisia waasi hawa walipata mafunzo kutoka kwa wanajeshi na polisi wa zamani wa Msumbiji.

Baadae vita ya ndani viliungwa mkono kutoka nje ya taifa hilo.

Serikali ilileta askari kutoka nje wakati wanamgambo wakiwa wanapokea mafunzo ya kijeshi na dini huko Afrika Mashariki – wapiganaji wa Jihadi kutoka ughaibuni waliweka uhusiano na kundi la kigaidi la kiislamu la Islamic State.

Ramani ya Msumbiji eneo la Kaskazini mwa Msumbiji

Vita ya uhuru ya Frelimo ilianza Septemba 25, mwaka 1964 huko Chai, kilomita 60km magharibi mwa Mocimboa da Praia.

Frelimo ilikusanya wapiganaji wadogo kwa kutumia mbinu sawa kabisa na ile ambayo ilitumika wakati wa mapigano na utawala wa ukoloni wa wareno uliokuwa ukichukua utajiri wote na uhuru ndio uliohitajika zaidi.

Viongozi wawili wa vita ya uhuru, Alberto Chipande na Raimundo Pachinuapa, ambao wote wana umri wa miaka 81 sasa ,ni wanaume wenye nguvu sana huko Cabo Delgado.

Wote ni wanachama wa chama cha kisiasa cha Frelimo, chama kikuu kinachofanya maamuzi.

Lakini sasa wanakabiliwa na uvamizi wa waasi sawa kabisa na ule wa wakati wa wakoloni miaka 55 iliyopita.

Mwaka 2009 madini ya rubi ambayo ni miongoni mwa madini yenye thamani kubwa duniani iligunduliwa Montepuez na mwanzoni wachimbaji wa ndani ,wakulima na wafugaji walifaidika

Lakini makubaliano yalitolewa na bwana Pachinuapa kushirikiana na kampuni kubwa ya uchimbaji madini.

Maelfu ya wachimbaji wadogo na wakulima waliathirika vibaya sana.

Mwaka jana, Gemfields alikubali kulipa Euro milioni 5.8 ($7.5m) kumaliza kesi katika mahakama iliyopo London , kesi iliyopelekwa na watu 273 waliodai kuwa waliminywa haki za binadamu wakati wakichukua eneo hilo.

Madai hayo yalidai kuwa kampuni yake ilikiuka sheria za makazi za Msumbiji, alitangaza mwezi Agosti kuwa makazi ya raia 105 yalikuwa tayari kwa wanakijiji hao kuhamia.

Baada ya hapo mwaka 2010 moja ya eneo kubwa la gesi asilia barani Afrika iligunduliwa pwani ya Cabo Delgado.

Na watu wachache tu waliweza kufaidika na kampuni ya huduma ya gesi , wakati wananchi wakiwa wamesahaulika.Makundi ya kampeni ya mazingira kama Justica Ambiental alisema fidia iliyotolewa ilikuwa haitoshi.

Wakulima waliokuwa wanalima na kukuza mazao yao bila pembejeo zaidi ya majembe , wavuvi waliokuwa wakivua kwa kutumia boti ndogo na neti waliondolewa katika eneo hilo.

Vijana waliokuwa na elimu kidogo waliokuwa na matumaini ya unafuu wa maisha zaidi ya wazazi wao ambao hawana elimu walipoteza matumaini.

Wakati wa uhuru wa Msumbiji walipojaribu kufuata njia ya ujamaa ambayo ilipingwa na ughaibuni na kusababisha vita ya mwaka 1982-92 ambapo watu milioni moja walifariki.

Mwisho wa vita ya baridi ya mwaka 1992,mataifa ya ughaibuni walitumia waliyotumia Ulaya ili kubadilisha Msumbiji kufuata mbinu ya kibepari badala ya ujamaa.

Lakini ubepari ndio umeweza kujenga rasilimali ya taifa hilo – biashara ,mikataba, umiliki wa ardhi, amabayo iliyosababisha kundi la wachache kutengenezwa zaidi ya wafanyabiashara.

Hii ililazimisha ubinafsishaji wa mamia ya makampuni ya serikali, kupendelewa kwa jeshi na viongozi wa chama cha Frelimo.

Benki ya dunia ilikiri kutoa mkopo ambao alidhani utalipwa na makampuni hayo binafsi.

Mapema mwaka 2000 , watu wawili waliokuwa wanaongoza kampeni za kupinga rushwa waliuawa.

Baada ya muda mfupi, Msumbiji ilipokea dola milioni 122 (£94m) zaidi ya walichoomba kutoka kwa wafadhili katika mkutano.

Ajira zipo lakini sio kwa raia wa Msumbiji

Mwaka 2013-14 , maofisa wa juu waliomba mkopo mkubwa wa dola bilioni mbili $2bn kama rushwa -lakini wapatao 20 nchini Msumbiji wamekuwa wakiuelezea kuwa ni mkopo wa kisiri.

Mfadhili wa kwanza alijitoa.Lakini wakati ukubwa wa gesi ulipogundulika, wafadhili waliachana na mazungumzo ya serikali bora, kupunguza umasikini na kujikita katika uwekezaji wa kigeni.

Msumbiji ina waislamu asilimia 18 ya jamii ya nchi hiyo

Kulikuwa na upinzani kutoka jumuiya ya kimataifa wakati Frelimo iliposhutumiwa kuweka udhibiti katika uchaguzi wa mwaka 2019.

Julai 17, 2020 wakati dola bilioni $14.9 iliposainiwa katika ufadhili wa mradi wa gesi.

• Uingereza ilihaidi kufadhili dola bilioni moja $1bn, amabyo walijivunia kutoa msaada wa ajira 2,000 Uingereza.

• Wakati benki ya Marekani ilitoa mkopo wa dola bilioni nne nukta saba $4.7bn,ambazo zitasaidia ajira 16,700 nchini Marekani.

Mradi wa ujenzi utaajiri raia wa Msumbiji 2,500 peke yake

Idadi ambayo ni mara saba zaidi ya ajira zinazoanzishwa Marekani na Uingereza kutokana na rasilimali ya Msumbiji.

Ajira nyingi zilizopo Msumbiji , watakaopata sio watu kutoka Cabo Delgado.

Jambo ambalo haliwezi kumaliza hisia za kutengwa na kuzuia vijana wengi wa Cabo Delgado, kuendelea kujiunga na kundi la kigaidi.

Haya ni matokeo ya kushindwa na rasilimali kuonekana kuwa kama laana ambayo inaongeza umasikini na kuondoa usawa, lakini kwa faida na ajira za makampuni ya kigeni na fedha kwa wakuu wa serikalini katika chama cha Frelimo.

Msumbiji bado inatafuta suluhisho la wanamgambo. Na huku tayari wanajeshi wa Afrika Kusini wakiwa angani na helikopta , huku Ufaransa, Marekani na mataifa mengine yakihaidi kutoa msaada wa kijeshi.

Lakini hao hawawezi kutatua tatizo linalowakabili vijana ambao hawana matumaini, bila ya kueleza namna ajira zitapatikana na faida vilevile.

Source link

,Dakika 3 zilizopita Chanzo cha picha, Reuters Jeshi la Msumbiji linashindwa kuukomboa mji wa bandari kutoka wanamgambo wa kiislamu (IS),…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *