Wanamgambo na ‘laana’ ya utajiri wa gesi na madini ya rubi Msumbiji, on September 18, 2020 at 1:00 pm

September 18, 2020

 Jeshi la Msumbiji linashindwa kuukomboa mji wa bandari kutoka wanamgambo wa kiislamu (IS), mji huo ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza hifadhi kubwa ya gesi asilia barani Afrika-Kwa miaka mitatu taifa hilo limevamiwa na waasi na kufanya rasilimali hiyo kuwa laana nyingine katika nchi hiyo, anaandika mchambuzi wa Msumbiji Joseph Hanlon.Hatimaye rais Filipe Nyusi anakabiliwa na uhalisia wa laana ya rasilimali.Waasi wanaajiri wanachama wengine zaidi kwa kutumia udhaifu wa umasikini wa vijana Kaskazini mwa Msumbiji, alieleza katika hotuba yake hivi karibuni huko Pemba, mji mkuu mkuu wa Cabo DelgadoNa alikiri kuwa licha ya kuwa majimbo matatu ya kaskazini – Cabo Delgado, Niassa na Nampula – wana utajiri mzuri wa asilia na uwezo mkubwa katika kilimo, lakini wako katika kiwango cha juu cha umaskini.Kwa miaka 15, kipato cha ndani cha Msumbiji kiliongezeka kwa asilimia sita 6% kwa mwaka, ongezeko hilo likitokana na rasilimali asilia kama makaa ya mawe, utengenezwaji wa umeme wa nguvu ya maji,kemikali ya atomiki na rasilimali nyingine.Ingawa bado wananchi wengi wakiwa hawajafanikiwa na rasimili hizo, umasikini na kutokuwa na usawa vyote viliongezeka.Kugundulika kwa amana kubwa ya rubi na eneo kubwa la kuchimba gesi nyingi ya asilia huko Cabo Delgado mwaka 2009-10, kulileta matumaini ya ajira na maisha bora kwa wananchi wengi lakini matumani hayo yalipotea ghafla.Ilidaiwa kuwa faida ilikuwa inachukulitwa na kundi la wachache katika chama cha Frelimo ambacho kimetawala Msumbiji tangu taifa hilo lipate uhuru mwaka 1975.Chanzo cha kukua kwa uasi wa kundi la kiislamuVita iliyoanza Oktoba 05, mwaka 2017 wakati kundi la waasi walipoteka miji na bandari ya Mocimboa da Praia kwa muda wa siku mbili.Mji huo ulikuwa kilomita 60 kama maili 32 kusini kutoka katika mji wenye eneo kubwa la maendeleo ya gesi huko Palma na bandari ni muhimu kwa ajili ya mradi wa gesi kwa ajili ya kuisambaza.Uasi huo uligunduliwa na wakazi wa eneo hilo.Tangu wakati huo, vita iliongezeka na watu wapatao 1,500 waliuawa na wengine wapatao 250,000 walikimbia makazi yao.,

 

Jeshi la Msumbiji linashindwa kuukomboa mji wa bandari kutoka wanamgambo wa kiislamu (IS), mji huo ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza hifadhi kubwa ya gesi asilia barani Afrika-Kwa miaka mitatu taifa hilo limevamiwa na waasi na kufanya rasilimali hiyo kuwa laana nyingine katika nchi hiyo, anaandika mchambuzi wa Msumbiji Joseph Hanlon.

Hatimaye rais Filipe Nyusi anakabiliwa na uhalisia wa laana ya rasilimali.

Waasi wanaajiri wanachama wengine zaidi kwa kutumia udhaifu wa umasikini wa vijana Kaskazini mwa Msumbiji, alieleza katika hotuba yake hivi karibuni huko Pemba, mji mkuu mkuu wa Cabo Delgado

Na alikiri kuwa licha ya kuwa majimbo matatu ya kaskazini – Cabo Delgado, Niassa na Nampula – wana utajiri mzuri wa asilia na uwezo mkubwa katika kilimo, lakini wako katika kiwango cha juu cha umaskini.

Kwa miaka 15, kipato cha ndani cha Msumbiji kiliongezeka kwa asilimia sita 6% kwa mwaka, ongezeko hilo likitokana na rasilimali asilia kama makaa ya mawe, utengenezwaji wa umeme wa nguvu ya maji,kemikali ya atomiki na rasilimali nyingine.

Ingawa bado wananchi wengi wakiwa hawajafanikiwa na rasimili hizo, umasikini na kutokuwa na usawa vyote viliongezeka.

Kugundulika kwa amana kubwa ya rubi na eneo kubwa la kuchimba gesi nyingi ya asilia huko Cabo Delgado mwaka 2009-10, kulileta matumaini ya ajira na maisha bora kwa wananchi wengi lakini matumani hayo yalipotea ghafla.

Ilidaiwa kuwa faida ilikuwa inachukulitwa na kundi la wachache katika chama cha Frelimo ambacho kimetawala Msumbiji tangu taifa hilo lipate uhuru mwaka 1975.

Chanzo cha kukua kwa uasi wa kundi la kiislamu

Vita iliyoanza Oktoba 05, mwaka 2017 wakati kundi la waasi walipoteka miji na bandari ya Mocimboa da Praia kwa muda wa siku mbili.

Mji huo ulikuwa kilomita 60 kama maili 32 kusini kutoka katika mji wenye eneo kubwa la maendeleo ya gesi huko Palma na bandari ni muhimu kwa ajili ya mradi wa gesi kwa ajili ya kuisambaza.

Uasi huo uligunduliwa na wakazi wa eneo hilo.

Tangu wakati huo, vita iliongezeka na watu wapatao 1,500 waliuawa na wengine wapatao 250,000 walikimbia makazi yao.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *