Wanajeshi 3 wa Pakistan wauawa katika shambulizi, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on August 31, 2020 at 3:00 pm

August 31, 2020

Wanajeshi watatu wa Pakistan wameuawa baada ya kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wakati wa harakati za kuitafuta ngome kuu ya kundi la Taliban na al-Qaida kaskazini magharibi karibu na mpaka wa Afghanistan. Jeshi la Pakistan limesema wanajeshi wengine wanne wamejeruhiwa katika shambulizi hilo la Waziristan Kusini, wilaya iliyoko kwenye jimbo la Khyber Pakhtunkhwa. Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo, ingawa kundi la Taliban nchini Pakistan limelaumiwa kwa mashambulizi kama hayo siku za nyuma kwenye eneo hilo, ambako wanamgambo wanaendesha shughuli zao. Kwa mujibu wa ripoti iliyozinduliwa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa, zaidi ya wanamgambo 6,000 wa Pakistan wamejificha Afghanistan. Wengi wa wapiganaji hao ni kutoka kwenye kundi la Taliban la Pakistan lililopigwa marufuku, ambalo mara nyingi hulishambulia jeshi la Pakistan na raia.,

Wanajeshi watatu wa Pakistan wameuawa baada ya kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wakati wa harakati za kuitafuta ngome kuu ya kundi la Taliban na al-Qaida kaskazini magharibi karibu na mpaka wa Afghanistan.

 Jeshi la Pakistan limesema wanajeshi wengine wanne wamejeruhiwa katika shambulizi hilo la Waziristan Kusini, wilaya iliyoko kwenye jimbo la Khyber Pakhtunkhwa. 

Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo, ingawa kundi la Taliban nchini Pakistan limelaumiwa kwa mashambulizi kama hayo siku za nyuma kwenye eneo hilo, ambako wanamgambo wanaendesha shughuli zao. 

Kwa mujibu wa ripoti iliyozinduliwa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa, zaidi ya wanamgambo 6,000 wa Pakistan wamejificha Afghanistan.

 Wengi wa wapiganaji hao ni kutoka kwenye kundi la Taliban la Pakistan lililopigwa marufuku, ambalo mara nyingi hulishambulia jeshi la Pakistan na raia.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *