Wanafunzi wa DA rasa la 4, Darasa la 8 na Kidato cha 4 Kurejea Shule Jumatatu Ijayo Kenya

October 6, 2020

Wizara ya Elimu imewataka wanafunzi wa Kidato cha Nne, Darasa la Nane na Darasa la Nne kurejea shuleni Jumatatu ijayo ili kukamilisha masomo ya muhula wa pili yatakayoendelea kwa wiki 11

Waziri wa Elimu amezitaka shule kuendelea kufuata kanuni za kudhibiti maambukizi ya #CoronaVirus kama vile kuvaa barakoa, kupima joto la Wanafunzi na Walimu, kunawa mikono na kudumisha hali ya usafi

Amesema, “Shule zote ambazo zilitumika kama vituo vya Karantini zimepuliziwa dawa ya kuua viini vya #COVID19 na kutayarisha madarasa kwaajili ya masomo”. Wanafunzi wataenda likizo ya wiki 1 Desemba 24, 2020 na kurejea tena Januari 4, 2021 kwa muhula wa 3

Mitihani ya Taifa ya KCPE na KCSE itafanyika Machi 22 hadi Machi 24, 2021 na Machi 25 hadi Aprili 4, 2021 mtawalia. Matokeo ya mtihani wa KCSE yatatangazwa hapo Mei 2021

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *