Wanafunzi sekondari waongezeka kutoka milioni 1.6 mpaka milioni 2.1,

October 5, 2020

 

Na Omary Mngindo, Bagamoyo

WANAFUNZI wa shule za Sekondari nchini wameongezeka kutoka milioni 1.6 mpaka kufikia milioni 2.1 ndani ya kipindi cha miaka mitano ya kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020.

Meneja wa Kampeni wa mgombea ubunge Jimbo la Bagamoyo Yahya Msonde ameyasema hayo kabla ya kuwaombea kura mgombea Urais Dkt. John Magufuli, ubunge Muharami Mkenge na diwani Apsa Kilingo katika uwanja wa TopTop Majani Mapana Kata Dunda.

Alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Rais Magufuli, kazi kubwa imefanyika, ikiwemo sekta ya elimu kwa kuwepo ongezeko kubwa la wanafunzi kuanzia msingi, sekondari mpaka vyuo, huku akisema katiia sekondari idadi kubwa imeongezeka.

“Leo nasimama hapa kukiombea kura chama changu, mgombea urais Dkt. John Magufuli ameweza kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu, ambapo kutoka mwaka 2015 mpaka 2020 wanafunzi wa sekondari wametoka milioni 1.6 mpaka milioni 2.1,” alisema Msonde.

Kwa upande wake Mkenge amewataka wana-Bagamoyo kuchangamkia mikopo inayotolewa na Serikali chini ya Chama Cha Mapinduzi CCM, ambayo ni isilimia kumi, ambapo nne vijana, nne wanawake na mbili makundi maalumu.

Ameeleza kwamba mikopo hiyo isiyo na riba inatolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kupitia mapato yake ya ndani hivyo amewataka kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiunga na kuanzisha vikundi hatimae wanufaike na fursa hiyo.

“Pamoja na juhudi kubwa zinazofanyika chini ya Serikali yetu inayoongozwana rais wetu mpendwa Dkt. John Magufuli lakini tunatambua bado kuna changamoto za hapa na pale katika sekta ya afya, ilani yetu inarleza kwamba tunakwenda kujenga Kituo cha afya kila Kata ba zaganati kila Kijiji,” alisema Mkenge.

Nae Kilingo ameomba ridhaa kwa wana-Majani Mapana wakichague chama hicho ili wamalizie kazi, huku akiongeza kuwa Serikali imeboresha sekta ya afya na kueleza kuwa vijana zaidi ya 100 waliokuwa wanatumia dawa za kulevya wamepatiwa tiba.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *