Wana- CCM 3,000 kumlaki Samia Chalinze, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 2), on September 2, 2020 at 3:00 pm

September 2, 2020

Na Omary Mngindo, Lugoba.WANACHAMA zaidi ya elfu tatu wanataraji kujitokeza kwenye viwanja vya Polisi Chalinze kumlaki Mgombea Mwenza wa Rais Mama Samia Suluu, atakapokuwa ziarani wilaya ya Bagamoyo kesho Septemba 3.Katika ziara hiyo Mama Samia ataanzia Chalinze asubuhi wakati mchana Bagamoyo, akiwa kwenye Kampeni ya kuwanadi wagombea Ubunge na Udiwani kwenye majimbo hayo mawili yaliyopo wilayani hapa.Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani hapa Alhaj Abdul Sharifu, akizungumza na Makatibu wa chama hicho kutoka Kata 15 zinazounda Halmashauri ya Chalinze, kikao kilichofanyika kwenye shule ya Sekondari Lugoba.”Hiki kikao ni mwendelezo wa vikao vyetu ambacho tangu kifunguliwe siku chache zilizopita, hakitafungwa mpaka siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi Oktoba 28, kikao chetu kitagungwa Oktoba 27,” alisema Sharifu.Alisemaa kwamba kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Serikali inayoongozwa na CCM chini ya Rais Dkt. John Magufuli, imefanya mambo mengi, huku akigusia miradi kadhaa iliyotekelezwa ndani ya wilaya ya Bagamoyo ikiwemo Mkoa mzima wa Pwani.Nae Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu alisema kuwa zawadi pekee ambayo wana-Bagamoyo wanatakiwa kuwapatia viongozi wa Serikali, mojawapo ya mapokezi ya nguvu kwa Mama Samia, na kwamba kujitokeza wao kutamuongezea imani zaidi kwa kiongozi huyo kwa wananchi hao.”Viongozi wetu wametufanyia mengi makubwa kwetu wana-Bagamoyo, tunajionea miradi inayoendelea kitekelezwa kila kukicha, hapa Chalinze tuna miradi kadhaa ukiwemo wa kimkakati wa maji, unaotokea chanzo cha Ruvu unaokuja Chalinze, Msoga mpaka Mboga, yote ni kuonesha imani yao kwetu,” alisema Mgalu.Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wilaya hiyo Lukhia Masenga aliwaomba akina-Mama kujitokeza kwa wingi, huku akiwahimoza kuzingatia muda kwani msafara utakapowakura njiani hawatoweza kumlaki Mwanamke mwenzao.”Tujitahidi mpaka ikifika saa 2 tuwe tumeahafika kwenye viwanja vya nyuma ya Polisi, ili tuweze kumlaki kiongozi wetu Mama Samia Suluu atayekuja kuungana nasi katika zoezi la kampeni iliyozinduliwa Miono na Katibu Mkuu wetu Mstaa Abdurhamani Kinana,” alisema Masenga.Awalo akifungua kikao hicho, Katibu wa chama hicho Gertrude Sinyinza alisema kuwa wana-CCM wana kila sababu gaa kitembea kifua mbele kutokana na kazi kubwa inayotekelezwa na Serikali inayoongozwa na Dkt. John Magufuli inayosimamiwa na chama hicho.,

Na Omary Mngindo, Lugoba.

WANACHAMA zaidi ya elfu tatu wanataraji kujitokeza kwenye viwanja vya Polisi Chalinze kumlaki Mgombea Mwenza wa Rais Mama Samia Suluu, atakapokuwa ziarani wilaya ya Bagamoyo kesho Septemba 3.

Katika ziara hiyo Mama Samia ataanzia Chalinze asubuhi wakati mchana Bagamoyo, akiwa kwenye Kampeni ya kuwanadi wagombea Ubunge na Udiwani kwenye majimbo hayo mawili yaliyopo wilayani hapa.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani hapa Alhaj Abdul Sharifu, akizungumza na Makatibu wa chama hicho kutoka Kata 15 zinazounda Halmashauri ya Chalinze, kikao kilichofanyika kwenye shule ya Sekondari Lugoba.

“Hiki kikao ni mwendelezo wa vikao vyetu ambacho tangu kifunguliwe siku chache zilizopita, hakitafungwa mpaka siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi Oktoba 28, kikao chetu kitagungwa Oktoba 27,” alisema Sharifu.

Alisemaa kwamba kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Serikali inayoongozwa na CCM chini ya Rais Dkt. John Magufuli, imefanya mambo mengi, huku akigusia miradi kadhaa iliyotekelezwa ndani ya wilaya ya Bagamoyo ikiwemo Mkoa mzima wa Pwani.

Nae Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu alisema kuwa zawadi pekee ambayo wana-Bagamoyo wanatakiwa kuwapatia viongozi wa Serikali, mojawapo ya mapokezi ya nguvu kwa Mama Samia, na kwamba kujitokeza wao kutamuongezea imani zaidi kwa kiongozi huyo kwa wananchi hao.

“Viongozi wetu wametufanyia mengi makubwa kwetu wana-Bagamoyo, tunajionea miradi inayoendelea kitekelezwa kila kukicha, hapa Chalinze tuna miradi kadhaa ukiwemo wa kimkakati wa maji, unaotokea chanzo cha Ruvu unaokuja Chalinze, Msoga mpaka Mboga, yote ni kuonesha imani yao kwetu,” alisema Mgalu.

Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wilaya hiyo Lukhia Masenga aliwaomba akina-Mama kujitokeza kwa wingi, huku akiwahimoza kuzingatia muda kwani msafara utakapowakura njiani hawatoweza kumlaki Mwanamke mwenzao.

“Tujitahidi mpaka ikifika saa 2 tuwe tumeahafika kwenye viwanja vya nyuma ya Polisi, ili tuweze kumlaki kiongozi wetu Mama Samia Suluu atayekuja kuungana nasi katika zoezi la kampeni iliyozinduliwa Miono na Katibu Mkuu wetu Mstaa Abdurhamani Kinana,” alisema Masenga.

Awalo akifungua kikao hicho, Katibu wa chama hicho Gertrude Sinyinza alisema kuwa wana-CCM wana kila sababu gaa kitembea kifua mbele kutokana na kazi kubwa inayotekelezwa na Serikali inayoongozwa na Dkt. John Magufuli inayosimamiwa na chama hicho.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *