Wamorocco waandamana kupinga mauhusiano ya kidiplomasia ya mataifa ya Kiarabu na Israel, on September 19, 2020 at 6:00 pm

September 19, 2020

 Pamoja na uwepo wa marufuku ya kufanyika mikusanyiko mikubwa kwa lengo la kukabiliana na janga la virusi vya corona, idadi kubwa ya waaandamanaji wamekusanyika nje ya jengo la bunge la Morocco kulaani kitendo cha mataifa ya Kiarabu kuridhia mahusiano na Israel. Katika mpango unaosimamiwa na Marekani, Jumanne iliyopita Israel ilitia saini makubaliano ya kihistoria ya kidiplomasia na Jumuiya ya Falme za Kiarabu na Bahrain. Morocco imeripotiwa ni moja kati ya mataifa ya Kiarabu ambayo yanatazamiwa kuchukua hatua kama hiyo, ingawa waziri mkuu alikanusha mwezi uliopita. Waandamanaji katika mji mkuu wa Morocco, Rabat, walipeperusha bendera ya Palestina huku wakiimba maneno yenye kukikemea kitendo hicho kwa kusema sawa na usaliti na kwamba Palestina sio ya kuuzwa.,

 

Pamoja na uwepo wa marufuku ya kufanyika mikusanyiko mikubwa kwa lengo la kukabiliana na janga la virusi vya corona, idadi kubwa ya waaandamanaji wamekusanyika nje ya jengo la bunge la Morocco kulaani kitendo cha mataifa ya Kiarabu kuridhia mahusiano na Israel. 

Katika mpango unaosimamiwa na Marekani, Jumanne iliyopita Israel ilitia saini makubaliano ya kihistoria ya kidiplomasia na Jumuiya ya Falme za Kiarabu na Bahrain. Morocco imeripotiwa ni moja kati ya mataifa ya Kiarabu ambayo yanatazamiwa kuchukua hatua kama hiyo, ingawa waziri mkuu alikanusha mwezi uliopita. 

Waandamanaji katika mji mkuu wa Morocco, Rabat, walipeperusha bendera ya Palestina huku wakiimba maneno yenye kukikemea kitendo hicho kwa kusema sawa na usaliti na kwamba Palestina sio ya kuuzwa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *