Wamiliki na walezi wa vituo vya watoto wapewa mafunzo maalumu, on September 10, 2020 at 10:00 am

September 10, 2020

Na Hamisi Nasri, Masasi   WAMILIKI na walezi wa vituo vya malezi ya watoto waliochini ya miaka mitano katika Halmashauri ya mji Masasi mkoani Mtwara,wamepatiwa mafunzo maalumu kwa lengo la kufahamu sheria,kanuni na miongozo ya uendeshaji wa vituo hivyo.  Mafunzo hayo ya siku tatu yamefanyika mjini Masasi na kuratibiwa na uongozi wa Halmashauri ya mji Masasi kupitia idara ya ustawi wa jamii yakilenga kutoa elimu kwa washiriki hao  zaidi ya 50 ambao ni wamiliki na walezi wa vituo hivyo kuweza na uwelewa wa kutosha juu ya miongozo ya serikali katika kulea watoto na kuwasimamia wanapokuwa kwenye vituo hivyo.   Akisoma taarifa fupi kuhusu mafunzo hayo jana wakati wafunga mafunzo, Mratibu wa Mafunzo, ambaye ni afisa ustawi wa jamii Halmashauri ya mji Masasi, Marcel  Kaijage alisema kwa mujibu wa kanuni za mwaka 2014 sura ya 13 kupitia sharia ya mtoto ya namba 21 ya mwaka 2009 ulipaswa kufanya ukaguzi wa vituo hivyo.  Kaijage alisema lengo la kufanya ukaguzi huo ni kuangalia kama wamiliki na walezi wa vituo hivyo vya kulelea watoto wanafuata sheria,kanuni na miongozo iliyowekwa na serikali, na baada ya ukaguzi huo walibaini baadhi ya changamoto ikiwemo vituo na walezi kukosa sifa zinazostahili.   Alisema kuwa baadhi ya changamoto ambazo zilibainika mara baada ya kufanya ukaguzi huo ni jamii kutohamasika kupeleka watoto kwenye vituo vya kulelea watoto, baadhi ya vituo kufunguliwa bila ya kufuata utaratibu, vituo kusitisha huduma kabla ya muda, vituo kuwa na idadi kubwa ya watoto tofauti na idadi ya walezi,  Kaijage alisema changamoto nyingine ni vituo kukosa huduma ya maji safi na salama,walimu kukosa sifa stahiki zinazotakiwa kwa mwalimu wa kulelea watoto, vituo kukosa huduma ya kwanza, ukosefu wa huduma za michezo, wahudumu wa mapishi kutofuata utaratibu wa vipimo vya afya,uhaba wa vyoo na magodoro ya kumpuzika kuchakaa au kukosekana kabisa.   Aidha,Kaijage alisema changamoto nyingine kukosekana kwa kamati za shule pamoja na ukosefu wa mbao za matangazo, baadhi ya vituo kuwa na watoto ambao wamezidi umri wa miaka mitano jambo ambalo ni kinyume na sheria, ukosefu wa sare kwa watoto na walimu wenyewe pamoja na ukosefu wa ofisi za vituo.  Alisema hivyo mafunzo hayo kwa sasa yatatoa mwanga kwa wamiliki na walezi hao wa vituo kuanza kutambua sheria na kanunu za uendeshaji wa vituo hivyo ili kila kituo hivi sasa kiwe kinaendeshwa kwa kufuata utaratibu. “Lengo la mafunzo haya ni kupunguza changamoto zilizopo kwenye vituo hivi vya kulelea watoto awali kabla ya kufanya ukaguzi wa vituo hivi kulikuwa na mambo kadhaa ambayo tumeyabaini ikiwemo baadhi ya vituo kuwa na idadi kubwa ya watoto huku vituo vingine vikiwa na watoto wenye umri zaidi ya miaka mitano,”alisema Kaijage     Alisema halamashauri ya mji Masasi inajumla ya vituo 43 ambapo kwa sasa vituo hivyo vimefanyiwa ukaguzi huku vituo 20 vikitumika kama mfano wa ukaguzi, jumla ya watoto ambao wamesajiliwa ni 2875 wamesajiliwa kwa mwaka wa masomo 2020/2021 huku lengo usajili wa watoto ni kufikia jumla ya watoto 17,280 walioko chini ya miaka mitano.  Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo ya mji, mwanasheria wa halmshauri hiyo, Joseph Mbungu aliwasihi washiriki wa mafunzo hayo kufuata sheria zilizopo za uendeshaji wa vituo hivyo ili aweze shughuli zao zitambulike kisheria.   Naye mmoja wa washiriki hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Diana alisema kuwa wanaupongeza uongozi wa halmashauri idara ya ustawi wa jamii kwa kuamua kutoa mafunzo hayo muhimu na kwamba kwa wametambua kanuni, sheria na miongozo ya uendeshaji wa vituo vya kulelea watoto na kwamba kwa sasa watafuata sheria zote zinazotakiwa.  Washiriki hao pia wamepatiwa vyeti maalumu vya kuhitimu mafunzo hayo ikiwa na kuwatumbua kama wametambua umuhimu na sheria za uendeshaji wa vituo hivyo vya kulelea watoto.,

Na Hamisi Nasri, Masasi 

  WAMILIKI na walezi wa vituo vya malezi ya watoto waliochini ya miaka mitano katika Halmashauri ya mji Masasi mkoani Mtwara,wamepatiwa mafunzo maalumu kwa lengo la kufahamu sheria,kanuni na miongozo ya uendeshaji wa vituo hivyo.

  Mafunzo hayo ya siku tatu yamefanyika mjini Masasi na kuratibiwa na uongozi wa Halmashauri ya mji Masasi kupitia idara ya ustawi wa jamii yakilenga kutoa elimu kwa washiriki hao  zaidi ya 50 ambao ni wamiliki na walezi wa vituo hivyo kuweza na uwelewa wa kutosha juu ya miongozo ya serikali katika kulea watoto na kuwasimamia wanapokuwa kwenye vituo hivyo.

   Akisoma taarifa fupi kuhusu mafunzo hayo jana wakati wafunga mafunzo, Mratibu wa Mafunzo, ambaye ni afisa ustawi wa jamii Halmashauri ya mji Masasi, Marcel  Kaijage alisema kwa mujibu wa kanuni za mwaka 2014 sura ya 13 kupitia sharia ya mtoto ya namba 21 ya mwaka 2009 ulipaswa kufanya ukaguzi wa vituo hivyo.

  Kaijage alisema lengo la kufanya ukaguzi huo ni kuangalia kama wamiliki na walezi wa vituo hivyo vya kulelea watoto wanafuata sheria,kanuni na miongozo iliyowekwa na serikali, na baada ya ukaguzi huo walibaini baadhi ya changamoto ikiwemo vituo na walezi kukosa sifa zinazostahili.

   Alisema kuwa baadhi ya changamoto ambazo zilibainika mara baada ya kufanya ukaguzi huo ni jamii kutohamasika kupeleka watoto kwenye vituo vya kulelea watoto, baadhi ya vituo kufunguliwa bila ya kufuata utaratibu, vituo kusitisha huduma kabla ya muda, vituo kuwa na idadi kubwa ya watoto tofauti na idadi ya walezi,

  Kaijage alisema changamoto nyingine ni vituo kukosa huduma ya maji safi na salama,walimu kukosa sifa stahiki zinazotakiwa kwa mwalimu wa kulelea watoto, vituo kukosa huduma ya kwanza, ukosefu wa huduma za michezo, wahudumu wa mapishi kutofuata utaratibu wa vipimo vya afya,uhaba wa vyoo na magodoro ya kumpuzika kuchakaa au kukosekana kabisa.

   Aidha,Kaijage alisema changamoto nyingine kukosekana kwa kamati za shule pamoja na ukosefu wa mbao za matangazo, baadhi ya vituo kuwa na watoto ambao wamezidi umri wa miaka mitano jambo ambalo ni kinyume na sheria, ukosefu wa sare kwa watoto na walimu wenyewe pamoja na ukosefu wa ofisi za vituo.

  Alisema hivyo mafunzo hayo kwa sasa yatatoa mwanga kwa wamiliki na walezi hao wa vituo kuanza kutambua sheria na kanunu za uendeshaji wa vituo hivyo ili kila kituo hivi sasa kiwe kinaendeshwa kwa kufuata utaratibu.

 “Lengo la mafunzo haya ni kupunguza changamoto zilizopo kwenye vituo hivi vya kulelea watoto awali kabla ya kufanya ukaguzi wa vituo hivi kulikuwa na mambo kadhaa ambayo tumeyabaini ikiwemo baadhi ya vituo kuwa na idadi kubwa ya watoto huku vituo vingine vikiwa na watoto wenye umri zaidi ya miaka mitano,”alisema Kaijage 

    Alisema halamashauri ya mji Masasi inajumla ya vituo 43 ambapo kwa sasa vituo hivyo vimefanyiwa ukaguzi huku vituo 20 vikitumika kama mfano wa ukaguzi, jumla ya watoto ambao wamesajiliwa ni 2875 wamesajiliwa kwa mwaka wa masomo 2020/2021 huku lengo usajili wa watoto ni kufikia jumla ya watoto 17,280 walioko chini ya miaka mitano.

  Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo ya mji, mwanasheria wa halmshauri hiyo, Joseph Mbungu aliwasihi washiriki wa mafunzo hayo kufuata sheria zilizopo za uendeshaji wa vituo hivyo ili aweze shughuli zao zitambulike kisheria.

   Naye mmoja wa washiriki hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Diana alisema kuwa wanaupongeza uongozi wa halmashauri idara ya ustawi wa jamii kwa kuamua kutoa mafunzo hayo muhimu na kwamba kwa wametambua kanuni, sheria na miongozo ya uendeshaji wa vituo vya kulelea watoto na kwamba kwa sasa watafuata sheria zote zinazotakiwa.

  Washiriki hao pia wamepatiwa vyeti maalumu vya kuhitimu mafunzo hayo ikiwa na kuwatumbua kama wametambua umuhimu na sheria za uendeshaji wa vituo hivyo vya kulelea watoto.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *