Wakuu wa shule Kenya watahadharishwa dhidi ya kuwanyunyizia ‘dawa’ wanafunzi,

October 14, 2020

Wizara ya afya nchini Kenya imewatahadharisha viongozi wa shule dhidi ya kuwanyungizia wanafunzi dawa za kuua vijidudu kama sehemu ya hatua za kukabiliana na virusi vya corona.

Wanafunzi wanaojiandaa kwa mitihani ya kitaifa katika shule za msingi na upili(sekondari) walirejea shuleni Jumatatu kwa masomo baada ya kukatiza masomo miezi takriban saba kufuatia mlipuko wa Covid-19.

Video inayoonesha wasichana wa shule waliojipanga msururu kwa ajili ya kunyunyiziwa dawa iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter wa gazeti nchini humo iliibua hasira.

Afisa wa utawala katika wizara ya afya Rashid Aman, amesema kuwa kemikali iliyotumiwa haifai kwa binadamu. Amesema, wizara itaagiza shule kuacha kuwanyungizia dawa wanafunzi.

Miongozo ya Shirika la afya duniani haishauri kuwanyunyizia watu dawa kwani unyunyiziaji huo unaweza kuwasababishia madhara ya kiafya.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *