Wakulima waadhimisha siku ya chakula Tanzania,

October 16, 2020

Wakulima waadhimisha siku ya chakula Tanzania Dunia hii leo inaadhimisha siku ya chakula ambapo wadau mbalimbali ikiwemo wakulima, wataalamu wa lishe bora, watafiti na maafisa ugani wanakutana leo jijini Dodoma katikati mwa Tanzania kwa lengo la kuangazia suala la upatikanaji wa chakula na lishe bora.

Ingawa katika baadhi ya maeneo nchini Tanzania, licha ya chakula kupatikana kwa wingi lakini bado kuna tatizo la utapiamlo.

Pelagia Gaudence ambae ni mkulima kutoka Arusha amesema tatizo kubwa la utapiamlo linasababoshwa na ukosefu wa elimu katika jamii kuhusu lishe bora.

Wakati huo huo, Elibarika Joseph ambae pia ni mkulima anasema kukosa elimu ya lishe bora kumemfanya amekuwa miongoni mwa waathirika wa lishe bora kutokana na ulaji wake kutozingatia virutubisho vinavyotakiwa.

Baadhi ya wakulima waliohudhuria kongamano hilo wameonekana kutilia mkazo matumizi ya mbegu za asili

Baadhi ya wakulima waliohudhuria kongamano hilo wameonekana kutilia mkazo matumizi ya mbegu za asiliImage caption: Baadhi ya wakulima waliohudhuria kongamano hilo wameonekana kutilia mkazo matumizi ya mbegu za asili

Maadhimisho Haya pia ya naenda sambamba na miaka 75 ya shirika la chakula duniani FAO. Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa zaidi ya nusu ya watu duniani hushiriki kizalisha chakula, lakini chini ya nusu ya watu duniani hupata chalula bora.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *