Wakimbizi 300 nchini Ugiriki wapelekwa katika kambi ya muda, on September 13, 2020 at 5:00 pm

September 13, 2020

Takribani wahamiaji 300 ambao walikuwa wanaishi katika kambi iliyoungua moto ya Lesbos, Ugiriki ya Moria wamehamishiwa katika eneo lingine la kambi ya muda.Televisheni ya Ugiriki imenukuu maafisa wakiwalekeza wahamiajia hao kwamba kila mmoja anapaswa kufanya vipimo vya haraka vya virusi vya corona, zoezi ambalo hata hivyo liliweza kubaini maambukizi saba.Kwa mujibu wa wizara ya afya wale waliobainika walipelekwa katika maeneo ya kujitenga. Kwa upande wa shughuli za uhamaji, mamlaka inaendelea kutafuta maeneo mengine ya kujenga kambi.Wahamiaji wengi wamekuwa wakishinikiza wapelekwe katika eneo la mataifa ya Ulaya Magharibi.Zaidi ya wakimbizi 12,000 walikuwa wanaishi katika kambi ya Moria, iliyokuwa na msongamano mkubwa wa watu kabla ya kuchomwa moto kutokana na vurugu kambini hapo.,

Takribani wahamiaji 300 ambao walikuwa wanaishi katika kambi iliyoungua moto ya Lesbos, Ugiriki ya Moria wamehamishiwa katika eneo lingine la kambi ya muda.

Televisheni ya Ugiriki imenukuu maafisa wakiwalekeza wahamiajia hao kwamba kila mmoja anapaswa kufanya vipimo vya haraka vya virusi vya corona, zoezi ambalo hata hivyo liliweza kubaini maambukizi saba.

Kwa mujibu wa wizara ya afya wale waliobainika walipelekwa katika maeneo ya kujitenga. Kwa upande wa shughuli za uhamaji, mamlaka inaendelea kutafuta maeneo mengine ya kujenga kambi.

Wahamiaji wengi wamekuwa wakishinikiza wapelekwe katika eneo la mataifa ya Ulaya Magharibi.

Zaidi ya wakimbizi 12,000 walikuwa wanaishi katika kambi ya Moria, iliyokuwa na msongamano mkubwa wa watu kabla ya kuchomwa moto kutokana na vurugu kambini hapo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *