Wakazi Ruvu wamliza Mwakamo,

October 17, 2020

WAKAZI wa Kijiji cha Ruvu Minazi Mikinda Kata ya Ruvu Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, wamemtoa machozi mgombea Ubunge Jimbo hilo Michael Mwakamo, baada ya kamkabidhi shilingi 115,000.

Tukio hilo lililofanyika jana baada ya wakazi kijijini hapo ambapo ndiko alikozaliwa Mwakamo, kuona ugumu wa zoezi la Kampeni za kuwani nafasi hiyo, ndipo wakaona uwepo wa haja ya kuchangishana kila mmoja hatimae kupatikana kwa kiwango hicho.

Akizungumza kabla ya kumkabidhi fedha hizo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata hiyo Juma Kidagala alisema kuwa, kuna dhana yaliyojengeka kwamba mbunge ndio anayepaswa kutoa pesa kila kukicha, mtazamo ambao wana-Ruvu wanapingana nao.

“Mwakamo ni mtoto wetu, amezaliwa Ruvu na hata utakampomfika umauti atazikwa hapa, isitoshe tunatambua kuwa ni mtumishi wa Serikali hivyo kulingana na uteuzi huu anakabiliwa na changamoto kubwa, tumechangisha kiasi kidogo japo uweke mafuta yatayokufikisha Mlandizi,” alisema Kidagala.

Baada ya kukabidhiwa kiwango hicho Mwakamo alianza kububujikwa machozi, kutokana na mapenzi makubwa ya wana-Ruvu hao dhidi yake, kabla ya kuwashukuru kwa moyo waliouonesha kwake, huku akiahidi kwamba hatowaangusha.

“Ninawashukuru sana wazazi wangu, vijana awenzangu na wote mlioonesha mapenzi makubwa kwangu, pia niwashukuru kwa dua zenu mlizokuwa mnaniombea tangu nilipowaambia dhamira yangu ya kuingia katika kinyang’anyiro cha Ubunge,, tupo pamoja ninaahidi sintowaangusha” alisema Mwakamo.

Aliongeza kwa kuwaomba wana-Ruvu kuendelea kumuombea dua ili aweze kutimiza majukumu yake ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo hilo kwa uadilifu mkubwa pasipokuwa upendeleo wa aina yeyote, huku akisema kwamba atakuwa muadilifu katika nafasi hiyo.

Aidha amewaomba wakazi hao kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi Oktoba 28 kuwachagua wagombea wanaotokea chama hicho kwa kuanzia Urais Dkt. John Magufuli, ubunge Mwakamo na Chamba kuwa diwani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *