Wahuni wa Mjini Wampiga Carlinhos

October 5, 2020

 

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Carlos Carlinhos, amekutana na wahuni wa mtandaoni ambao wamemliza kwa kumuibia akaunti yake ya Instagram.

Carlinhos ambaye amejiunga na Yanga msimu huu, amekutana na balaa hilo ikiwa ni siku chache baada ya kuanza kuonesha cheche zake ndani ya Ligi Kuu Bara.

Dismas Ten ambaye yupo katika Kitengo cha IT ndani ya Yanga, ameposti taarifa iliyosema: “Mwizi, kibaka jambazi punde tu tunamtia mkononi, lakini kwa sasa unaweza kumfollow huyu mwamba kupitia @officialcarlinhos sasa hivi ili twende sambamba..! @officialcarlinhos imewekwa ulinzi wa kutosha.”

Ishu za watu mbalimbali kuibiwa akaunti zao mtandaoni imekuwa endelevu ambapo wapo wanaofanikiwa kuzikomboa na wengine kuzipoteza kabisa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *