Wafungwa Zaidi ya 200 Watoroka Gerezani Uganda…Wakimbilia Mlimani..

September 17, 2020

 ZAIDI ya wafungwa 200 wa Gereza la Singila, Moroto Kaskazini Mashariki mwa Uganda, wametoroka gerezani baada ya kufanikiwa kumuua askari mmoja katika majibizano makali ya risasi. Kamishna wa Magereza nchini Uganda, Johnson Byabashaija, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba wafungwa hao waliwazidi nguvu askari magereza na kufanikiwa kuvunja ghala la silaha ambapo waliiba bunduki 15 walizozitumia kufanikisha kutoroka kwao. Byabashaija amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na msako mkali kwenye Mlima Moroto walikotorokea wafungwa hao.,

 

ZAIDI ya wafungwa 200 wa Gereza la Singila, Moroto Kaskazini Mashariki mwa Uganda, wametoroka gerezani baada ya kufanikiwa kumuua askari mmoja katika majibizano makali ya risasi.

 

Kamishna wa Magereza nchini Uganda, Johnson Byabashaija, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba wafungwa hao waliwazidi nguvu askari magereza na kufanikiwa kuvunja ghala la silaha ambapo waliiba bunduki 15 walizozitumia kufanikisha kutoroka kwao.

 

Byabashaija amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na msako mkali kwenye Mlima Moroto walikotorokea wafungwa hao.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *