Wafahamu wasanii 5 waliozawadiwa kofia na Rais Magufuli kwenye kampeni, wakiwemo Alikiba, Diamond na Harmonize

September 16, 2020

Hawa ndio wasanii watano walibahatika kuzawadiwa kofia na Mh. Rais Magufuli wakati wa kampeni zake zinazoendelea mikoani. Tukio la msanii Alikiba la kupewa kofia leo limefanya idadi ya wasanii waliopewa kofia na Rais Magufuli kufika watano na kadri siku zinavyoenda huenda tukaona wasanii wengine wakapewa kofia na Rais kwani kampeni bado zinaendelea.Msanii wa kwanza kabisa ni Mrisho Mpoto na wapi ni Bnana Zoro, wasanii hawa wote wawili walipewa kofia na Rais Magufuli katika kampeni zake zilizofanyika mkoani Singida ambapo wote wawili walipewa kofia kwa wakati mmoja.Tukio la pili la msanii kupewa kofia ni Diamond Platnumz katika kampeni zilizofanyika mkoani Mwanza ambapo ndio tukio lilovuta hisia za watu wengi kutokana na Diamond alivyotoa shukrani kwa Rais hadi kupelekea kwenda kuihifadhi kofia hiyo kabatini.Tukio la tatu ni msanii Harmonize ambalo lilifanyika katika kampeni za mkoani Geita katika wilaya ya Chato ambali lilifanyika wiki hii siku ya jumatatu.Na tukio la nne ni la msanii Alikiba ambaye amepewa kofia yake mkoani Kagera wakati Mh. Rais anafanya kampeni za kuomba kura, kwahiyo Alikiba, Diamond Platnumz, Harmonize, Mrisho Mpoto na Banana Zoro ndio wasanii waliobahatika kupewa kofia na Rais Magufuli.Unahisi ni kwanini wasanii Alikiba, Diamond Platnumz na Harmonize matukio yao yamevuta hisia za watu wengi kuliko tukio la mjomba Mrisho Mpoto na mkongwe Banana Zoro -?,

Hawa ndio wasanii watano walibahatika kuzawadiwa kofia na Mh. Rais Magufuli wakati wa kampeni zake zinazoendelea mikoani. Tukio la msanii Alikiba la kupewa kofia leo limefanya idadi ya wasanii waliopewa kofia na Rais Magufuli kufika watano na kadri siku zinavyoenda huenda tukaona wasanii wengine wakapewa kofia na Rais kwani kampeni bado zinaendelea.

Msanii wa kwanza kabisa ni Mrisho Mpoto na wapi ni Bnana Zoro, wasanii hawa wote wawili walipewa kofia na Rais Magufuli katika kampeni zake zilizofanyika mkoani Singida ambapo wote wawili walipewa kofia kwa wakati mmoja.

Tukio la pili la msanii kupewa kofia ni Diamond Platnumz katika kampeni zilizofanyika mkoani Mwanza ambapo ndio tukio lilovuta hisia za watu wengi kutokana na Diamond alivyotoa shukrani kwa Rais hadi kupelekea kwenda kuihifadhi kofia hiyo kabatini.

Tukio la tatu ni msanii Harmonize ambalo lilifanyika katika kampeni za mkoani Geita katika wilaya ya Chato ambali lilifanyika wiki hii siku ya jumatatu.

Na tukio la nne ni la msanii Alikiba ambaye amepewa kofia yake mkoani Kagera wakati Mh. Rais anafanya kampeni za kuomba kura, kwahiyo Alikiba, Diamond Platnumz, Harmonize, Mrisho Mpoto na Banana Zoro ndio wasanii waliobahatika kupewa kofia na Rais Magufuli.

Unahisi ni kwanini wasanii Alikiba, Diamond Platnumz na Harmonize matukio yao yamevuta hisia za watu wengi kuliko tukio la mjomba Mrisho Mpoto na mkongwe Banana Zoro -?

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *