Waandishi ibueni habari za wanawake na vijana katika nyanja mbalimbali, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 3, 2020 at 1:00 pm

September 3, 2020

Na Faruku Ngonyani, Mtwara.Waandishi wa habari wametakiwa kuendelea kuibua na kupaza sauti za wanawake na watoto lakini pia vijana katika nyanja mbalimbali.Pia, endapo kama jamii itakuwa na uelewa juu ya madhara yatokanayo na ukatili ya kijinsia kwa wanawake na watoto itasaidia kila mmoja kuzifahamu na kuzitambua na kuwa Taifa lenye haki na usawa wa kijinsia pasipo ukatili.Wito huo umetolewa na Mhadhiri wa chuo Kikuu Huria (OUT), Libe Mathias  Choyo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari juu ya namna ya kuripoti taarifa za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wananawake na watoto.Kwa upande wa waandishi hao wa habari wmepokea wito huo huku wakiahidi kuibui taarifa hizo mara tu baada ya kukamilika mafunzo hayo yanayofayika ukumbi wa TCCIA Mkoani Mtwara..Mafunzo hayo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Mtwara (YOUNG REPORTERS) yanasimimiwa na Taasisi ya TADIO, TBI, DLAB na MTPC na kufadhiliwa na European Union(EU) kwa lengo la kuwawezesha kuibua na kuandika habari za kijamii zinazohusu ukatili wa kijinsi,vijana na kufahamu sharia sheria pamoja na maadili ya uandishi wa habari.,

Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Waandishi wa habari wametakiwa kuendelea kuibua na kupaza sauti za wanawake na watoto lakini pia vijana katika nyanja mbalimbali.

Pia, endapo kama jamii itakuwa na uelewa juu ya madhara yatokanayo na ukatili ya kijinsia kwa wanawake na watoto itasaidia kila mmoja kuzifahamu na kuzitambua na kuwa Taifa lenye haki na usawa wa kijinsia pasipo ukatili.

Wito huo umetolewa na Mhadhiri wa chuo Kikuu Huria (OUT), Libe Mathias  Choyo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari juu ya namna ya kuripoti taarifa za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wananawake na watoto.

Kwa upande wa waandishi hao wa habari wmepokea wito huo huku wakiahidi kuibui taarifa hizo mara tu baada ya kukamilika mafunzo hayo yanayofayika ukumbi wa TCCIA Mkoani Mtwara..

Mafunzo hayo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Mtwara (YOUNG REPORTERS) yanasimimiwa na Taasisi ya TADIO, TBI, DLAB na MTPC na kufadhiliwa na European Union(EU) kwa lengo la kuwawezesha kuibua na kuandika habari za kijamii zinazohusu ukatili wa kijinsi,vijana na kufahamu sharia sheria pamoja na maadili ya uandishi wa habari.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *