Waandamanaji elfu 10 wahudhuria mkutano dhidi ya hatua za corona Munich, on September 13, 2020 at 10:00 am

September 13, 2020

 Takriban watu elfu 10 waliandamana katika mji wa Munich jimboni Bavaria kupinga hatua zilizowekwa za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona. Idara ya polisi imesema Jumamosi kuwa idadi ya watu hao ni mara mbili zaidi ya ile iliyosajiliwa huku hafla kama hizo zikifanyika katika miji mingine ya Ujerumani.Matembezi kupitia Munich ambayo yalifanyika kabla ya mkutano huo wa hadhara yalifutiliwa mbali baada ya kuwavutia mamia ya watu wengine huku polisi ikisema hakuna hata mtu mmoja aliyevaa barakoa. Katika taarifa yake ya kila wiki kupitia mtandao, kansela wa Ujerumani Angela Merkel alitetea hatua za serikali dhidi ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona lakini akasisitiza kuwa yuko tayari kuzungumzia suala hilo. Aliongeza kuwa katika taifa hilo, kila mtu yuko huru kuyakosoa maamuzi hayo ya serikali na kwamba uhuru huo wa kuandamana kwa amani umewafanya watu wengi kuionea wivu Ujerumani huku akisubiria siku ya Umoja wa Mataifa ya demokrasia ya kimataifa siku ya Jumanne.,

 

Takriban watu elfu 10 waliandamana katika mji wa Munich jimboni Bavaria kupinga hatua zilizowekwa za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona. 

Idara ya polisi imesema Jumamosi kuwa idadi ya watu hao ni mara mbili zaidi ya ile iliyosajiliwa huku hafla kama hizo zikifanyika katika miji mingine ya Ujerumani.

Matembezi kupitia Munich ambayo yalifanyika kabla ya mkutano huo wa hadhara yalifutiliwa mbali baada ya kuwavutia mamia ya watu wengine huku polisi ikisema hakuna hata mtu mmoja aliyevaa barakoa. 

Katika taarifa yake ya kila wiki kupitia mtandao, kansela wa Ujerumani Angela Merkel alitetea hatua za serikali dhidi ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona lakini akasisitiza kuwa yuko tayari kuzungumzia suala hilo. 

Aliongeza kuwa katika taifa hilo, kila mtu yuko huru kuyakosoa maamuzi hayo ya serikali na kwamba uhuru huo wa kuandamana kwa amani umewafanya watu wengi kuionea wivu Ujerumani huku akisubiria siku ya Umoja wa Mataifa ya demokrasia ya kimataifa siku ya Jumanne.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *