Vyuo 15 na Sekondari 21 kupamba Nyerere Day Wilaya ya Mtwara,

October 12, 2020

 

Na Faruku Ngonyani, Mtwara

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mkaoni Mtwara kwa kushirikiana na Vyuo 15 na Shule 21 za Sekondari wamepanga kufanya maonesho mbali mbali Kuelekea siku ya kumbukumbu ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya kwanza wa Tanzania  Mwl.Hayati Julias Kambarage Nyerere siku ya Juma Tano Tarehe 14 Oktoba 2020.

Akizungumza na kamati ya maandalizi inayoandaa maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya amesema kuwa watatumia wanafunzi wa vyuo na Sekondari vilivyopo Wilayani Mtwara ili kushiriki michezo mbali mbali kuenzi siku hiyo maalumu ya kumkumbuka ya Mwl. Nyerere.

Aidha Kyobya amechukua fursa hiyo kwa kuwalika watimishi wote wa Halmashauri Tatu zilizopo Wilaya ya Mtwara kwa maana Halmashuri ya Manispaa Mtwara Mikindani,Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara pamoja na Halmashauri ya Mji wa Nanyamba ili waweze kushiriki michezo mbalimbali ya siku hiyo.

‘Sisi kwa kutambua umuhimu wa Mwal.Julias Kambarage Nyerere Baba wa Taifa imepita miaka 21 toka ametutoka lakini sisi kama wana Mtwara tumeona bora tuandae njia bora ya kumuenzi,kunesha kwamba yale aliyokuwa anayafanya bado yanaendelezwa na Dkt John Pombe Magufuli’

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa kwa siku hiyo ya kumbukizi ya Mwal.Nyerere wanafunzi wa Vyuo pamoja na wa Sekondari watapata fursa ya kushiriki michezo na kushindana mashindano mbalimbali katika viwanja vya TTC Kawaida vilivyopo Manispaa Mtwara Mikindani.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya siku ya kumbukizi ya Mwl. Nyerere Mwl Justin Ngimba ambaye ni Mkuu wa Chuo Cha Mtwara Kawaida (TTC) amesema kuwa kwa upande wao maandalizi yanaenda vizuri huku wamekwishawaandaa vijana watakuwa wanatoa burudani katika viwanja hvyo

Lakini pia ameongeza kuwa moja ya maandalii yaliyofanywa ni pamoja kuwaandaa wanafunzi wataonesha matendo na misemo mbali mbali ya hayati Mwl Julias kambarage Nyerere  na wacheza Bao mchezo ambao Mwl Nyrere alikuwa anapenda kuucheza enzi za uwahi wake.

Hayati Mwl Julias Kambarage Nyerere alifariki dunia tarehe 14 Otoba mwaka 1999 kumbukizi yake hufanyika kila inapofika Tarehe 14 Otoba ya kila mwaka.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *