Virusi vya corona: WHO yaripoti ongezeko la maambukizi mapya ndani ya saa 24

September 14, 2020

Saa 3 zilizopita

India ni ya pili kwa idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa limerekodi ongezeko maambukizi mapya ya virusi vya corona kwa muda wa siku moja na kupata vifo zaidi ya 5,500, na kufanya dunia kuwa na jumla ya vifo 917,417 vilivyotokana na mlipuko huo.

Ongezeko kubwa la maambukizi limeripotiwa kutoka India, Marekani na Brazil.

Duniani kote kuna zaidi ya wagonjwa milioni 28 waliothibitika kuwa na virusi vya corona na nusu ya idadi hiyo ni kutoka Marekani.

Rekodi ya siku moja ya maambukizi mapya ilikuwa ya Septemba 6, wakati WHO iliporipoti maambukizi mapya 306,857.

Ni wapi ambapo maambukizi yanaongezeka kwa kasi?

Kwa mujibu wa WHO,India imeripoti maambukizi mapya 94,372 siku ya Jumapili na kufuatia, Marekani imeripoti visa 45,523 na Brazil ikiwa ni 43,718.

Zaidi ya vifo vipya 1,000 vimerekodiwa Marekani na India wakati Brazil, watu 874 walikufa kutokana na magonjwa yenye uhusiano na Covid-19 ndani ya saa 24.

India ni ya pili kurekodi maambukizi makubwa zaidi duniani baada ya Marekani.

Wiki iliyopita iliripotiwa karibu milioni mbili ya maambukizi ya virusi vya corona mwezi Agosti, idadi kubwa kurekodiwa tangu mlipuko ulipoanza.

Taifa hilo lilishuhudia wastani wa maambukizi 64,000 kwa siku – huku 84% ya wastani wa maambukizi yote mwezi Julai kwa mujibu wa takwimu rasmi.

Ongezeko la vifo limefikia 1,000 kila siku tangu mwanzoni mwa mwezi Septemba.

Brazil imerekodi zaidi ya wagonjwa milioni nne wa virusi vya corona na kuwa ya tatu duniani kwa kiwango cha juu cha maambukizi.

Kuna idadi kubwa ya vifo kutokana na corona maeneo ya Amerika ya Kusini , kwa idadi ya vifo 131,000 mpaka sasa.

Marekani imerekodi karibu robo ya maambukizi ya virusi vya corona duniani -ni zaidi ya milioni sita. Ongezeko lilionekana kila siku mwezi Julai lakini idadi imeshuka tangu wakati huo.

Marekani ina idadi kubwa ya vifo vilivyotokana na virusi vya corona, kwa zaidi ya idadi ya vifo 194,000.

Hali ikoje maeneo mengine?

Mataifa ya ulaya, rekodi ya maambukizi bado inaongezeka kila siku huku kukiwa na hofu ya mlipuko mwingine kutokea.

Amri ya kutotoka nje imewekwa katika maeneo yenye maambukizi makubwa na watu wametakiwa kuvaa barakoa na kuzingatia kukaa kwa umbali.

Mataifa mengine virusi vinaonekana kuibuka tena kama Peru, Israel, Korea Kusini na Australia.

Jumapili, polisi nchini Australia katika jimbo la Victoria waliwakamata waandamanaji 70 kwa kukiuka sheria ya kukaa nyumbani .

Zaidi ya watu 250 waliudhuria katika maandamano hayo katika mji wa Melbourne, walikuwa wanawahamasisha watu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mpango wa nadharia kuhusu mlipuko.

Jimbo la Victoria limekuwa kitovu cha mlipuko wa maambukizi nchini Australia, huku kukiwa na maambukizi ya 75% na vifo 90% vilivyotokana na virusi vya corona.

Kwa sasa Israel imeweka amri mpya ya kuzuia watu kutoka nje kutokana na maambukizi kuongezeka. Makatazo makali yalitolewa Ijumaa- katika mwaka mpya wa wayahudi- na sheria hizo zitadumu kwa muda wa wiki tatu, mamlaka imeeleza.

Israel imethibitisha zaidi ya maambukizi 153,000 na vifo1,108 vilivyotokana na Covid-19, kwa mujibu wa takwimu ya chuo kikuu cha Johns Hopkins.

Source link

,Saa 3 zilizopita Chanzo cha picha, HINDUSTAN TIMES Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa limerekodi ongezeko maambukizi mapya ya…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *