Virusi vya corona: WHO kuweka kanuni za kupima dawa za mitishamba za Afrika

September 20, 2020

Dakika 5 zilizopita

Bottles of Covid-Organics

Maelezo ya picha,

Dawa ya mitishamba ya Covid ilizinduliwa nchini Madagascar mwezi Aprili baada ya kutumiwa na watuchini ya 20katika kipindi cha wiki tatu

Shirika la afya duniani (WHO) limekubali kanuni za kupima dawa za mitishamba za Afrika kwa ajili ya mapambano dhidi ya Covid-19.

Sayansi itakuwa ndio msingi wa vipimo hivyo kwa ajili ya usalama na ufanisi wa dawa ambazo zitaidhinishwa na , imesema WHO.

Madawa yoyote ya kienyeji ambayo yanaaminika kuwa yana ufanisi yanaweza kuharakishwa kutengenezwa kwa kiango kikubwa.

Rais wa Madagascar amekuwa akinadi dawa ya asili ambayo haijafanyiwa vipimo ambayo anasema inaweza kutibu virusi vya corona, licha ya onyo la WHO dhidi ya matumizi ya dawa hizo za mitishamba.

WHO ilisema kuwa kanuni mpya zinalenga kusaidia na kuwawezesha wanasayansi wa Afrika kufanya majaribio yanayofaa ya kimatibabu.

Hatua hiyo inakuja baada ya idadi ya wagonjwa waliothibitishwa duniani kupita milioni 30, huku vifo vyote vilivyothibitishwa duniani vikiwa zaidi ya 957,000. Barani Afrika zaidi ya watu milioni 1.3 wamepatwa na maambukizi ya corona na zaidi ya vifo 33,000 vimeripotiwa.

Chanjo 140 zenye uwezekano wa kuwa chanjo kamili ya Covid-19 zinatengenezwa kote duniani , huku makumi kadhaa ya chanjo hizo zikiwa tayari zinafayiwa vipimo katika kliniki za majaribio ya chanjo.

Kuharakishwa kwa utafiti

Sambamba na juhudi hizi, kliniki za majaribio ya awamu ya tatu zimepewa ruhusa ya kuendelea kutumia dawa za kiasili za Afrika.

Jopo la wataalamu, linalojumuisha WHO, Kituo chakudhibiti na kuzuwia magonjwa cha Muungano wa Afrika na tume ya Muungano wa Afrika ya masuala ya kijamii, wamekubaliana juu ya mpangilio wa shughuli hiyo.

Awamu ya tatu ya majaribio kwa kawaida hupima usalama na ufanisi wa dawa kwa kundi kubwa la watu wanaoshiriki.

“Kuidhinishwa kwa nyaraka za kiufundi kutahakikisha kwamba ushahidi wa pamoja wa kimatibabu wa ufanisi wa dawa hizo asili kwa ajili ya tiba ya Covid-19 unapatikana bila kukiuka usalama wake ,” amesema Profesa Motlalepula Gilbert Matsabisa, mwenyekiti wa jopo hilo la wataalamu

2px presentational grey line

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?

2px presentational grey line

“Mwanzo wa Covid-19, sawa na mlipuko wa Ebola magharibi mwa Africa, umeonesha haja ya kuimarisha mifumo ya afya na kuharakisha tafiti na kuendeleza mipango ya maendeleo ya tiba , ikiwa ni pamoja na dawa za asili ,” alisema daktari wa WHO Prosper Tumusiime katika taarifa.

Mwezi Aprili, Rais wa Madagascar Andry Rajoelina alizindua dawa ya mitishamba ya Covid-Organics, akisema kuwa ilikuwa ni dawa ya kinga . Ilifanyiwa majaribio kwa watu 20 kwa kipindi cha zaidi ya wiki tatu.

Bw. Rajoelina anaimani kinywaji hicho cha mchanganyiko wa miti shamba kinazuwia corona, licha ya nchi yake kuwa na watu 15,925 wenye maambukizi ya corona na watu 216 wamethibitishwa kufa kwa Covid-19 nchini humo.

Kinywaji hicho ambacho pia kimekwishatumwa katika makumi kadhaa ya nchi za Afrika kinatengenezwa na Taasisi ya utafiti ya Madagascar ka ajili ya mmea wapakanga- ambao pia ni moja ya viungo vya dawa inayotibu Malaria na mimea mingine ya Madagascar.

DktTumusiime amesema kuwa kupitia jukwaa la WHO la udhibiti wa viwango vya chanjo za Afrika, sasa kuna njia ya majaribio ya tiba ya dawa katika kanda ya Afrika ambayo itatathminiwa na kuidhinishwa katika kipindi cha chini ya siku 60.

Unaweza pia kusoma:

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

Virusi vya corona: Je, Madagascar wamepata dawa ya mitishamba kutibu virusi vya corona?

Source link

,Dakika 5 zilizopita Chanzo cha picha, AFP Maelezo ya picha, Dawa ya mitishamba ya Covid ilizinduliwa nchini Madagascar mwezi Aprili…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *