Virusi vya corona: Je itakuwaje ikiwa Trump atakuwa mgonjwa sana na kushindwa kutekeleza majukumu yake?

October 3, 2020

Dakika 8 zilizopita

Trump and Pence

Maelezo ya picha,

Rais Trump na Makamu wa rais Mike Pence walichaguliw arasmi na chama cha Republican mwezi Agosti

Ikiwa zimesalia wiki chache tu kabla ya uchaguzi wa urais Marekani, Donald Trump amethibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Hilo limezua swali gumu la kipi kitakachotokea ikiwa atashindwa kutekelza majukumu yake.

Je kampeni gani ambayo rais atakosa?

Bwana Trump anahitajika kujitenga kwa siku 10 kuanzia alipopimwa kuthibitisha ikiwa ana ugonjwa wa Covid- 19 yaani Oktoba mosi, kwahiyo bado anaweza kushiriki mdahalo wa pili wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba 15.

Mkutano uliopangwa kufanyika Florida Ijumaa ulifutwa.

Bwana Trump ana mikutano mingine iliyopangwa kipindi hiki ambayo sasa hivi itahitajika kuahirishwa au kufutwa.

Je ni kwa hali gani uchaguzi unaweza kucheleweshwa?

Kipindi cha rais Trump kujitenga bila shaka kina athari zake katika kampeni.

Na hivyo basi kuna swali lililoulizwa la ikiwa uchaguzi unaweza kucheleweshwa na je hilo linaweza kutokea vipi?

Uchaguzi wa urais kisheria unafanyika Jumanne baada ya Jumatatu ya kwanza ya Novemba, kila baada ya miaka minne – hivyo basi mwaka huu utafanyika Novemba 3.

Kubadilisha tarehe kutakuwa jukumu la wabunge na wala sio rais.

Pia kutahitaji kuwa na wingi wa kura katika mabunge yote mawili kuuunga mkono kubadilishwa kwa tarehe yoyote ile.

Uwezekano wa hilo ni mdogo, ikizingatiwa kwamba kutahitajika kuungwa mkono na bunge la wawakilishi ambalo linadhibitiwa na chama cha Democratic.

President Trump at first debate

Maelezo ya picha,

Rais Trump alibeba barakoa kwenye mdahalo wa kwanza wa urais lakini hakuwahi kupigwa picha kama ameivaa

Hata kama utabadilishwa, sheria ya katiba ya Marekani inasema utawala wa rais unakuwa madarakani kwa miaka minne pekee. Hivyo basi, muhula wa rais utafika ukomo wake moja kwa moja Januari 20, 2021.

Na kubadilisha tarehe hii kutahitaji mabadiliko ya katiba. Hilo litahitajika kuidhinishwa na theluthi mbili ya wabunge, kisha robo tatu ya majimbo ya Marekani – hatua ambayo tena ni vigumu kufikiwa.

Je ni kipi kitakachotokea ikiwa rais atakuwa mgonjwa sana?

Ikiwa pengine rais atakuwa mgonjwa sana na kushindwa kutekeleza majukumu yake, katiba ya Marekani inasema hivi:

Marekebisho ya 25 yanaruhusu rais kukabidhi madaraka kwa makamu wake, ambaye kwa sasa ni Mike Pence atakayekuwa ana kaimu.

Na rais akipona, atachukua tena majukumu yake.

Trump and Marine One

Maelezo ya picha,

Rais Trump alipanda helikopta hiyo hiyo na Hope Hicks Jumatano. Hicks baadae alithibitshwa kupata maambukizi ya virusi vya corona

Ikiwa pengine rais atakuwa mgonjwa sana kiasi cha kushindwa kukabidhi madaraka, baraza la mawaziri na makamu wake wanaweza kumtangaza kwamba ameshindwa kuendelea kutekeleza majukumu na Bwana Pence ataanza kutekeleza majumu hayo.

Ikiwa Bwana Pence pia naye atashindwa kuetekeleza majukumu, chini ya Sheria ya Urithi wa Rais, Nancy Pelosi, spika wa Bunge la Wawakilishi – ambaye ni wa chama cha Democrat – ndiye anayefuata kwa orodha hiyo, ingawa wataalamu wa katiba wanasema uhamishaji wa madaraka wa namna hiyo utasababisha malumbano ya kisheria.

Na ikiwa naye hayuko tayari au hawezi kuendeleza majuku hayo, yatakabidhiwa Seneta mwandamizi wa chama cha Republican, ambaye kwa sasa ni Charles E Grassley, 87. Lakini hatua hiyo vilevile, moja kwa moja itakabiliwa na upinzani wa kisheria.

Graphic showing the key characters - Trump, Pence, Pelosi and Grassley

Je kipindi cha nyuma kuna rais amewahi kuumwa sana?

Mwaka 1985, rais Ronald Reagan alikuwa hospitalini alikofanyiwa upasuaji wa saratani na wakati huo alimkabidhi makamu wake, George HW Bush, madaraka.

Mwaka 2002 na 2007, Rais George W Bush alifanya vivyo hivyo kwa makamu wake baada ya kupata matibabu ya utumbo mpana .

Ikiwa Trump atashindwa kusimama kwenye uchaguzi, je ni jina la nani litakalokuwa kwenye kura?

Ikiwa kwa sababu yoyote ile, mgombea aliyechaguliwa na chama kama mgombea wao atashindwa kutekeleza jukumu hilo, kuna mchakato ulio wazi wa kufuatwa.

Ingawa makamu rais Mike Pence kwanza ataanza kutekelza majukumu ya rais, yeye hatakuwa mgombea wa chama cha Republican moja kwa moja – kwasababu tayari kuna mgombea ambaye amechaguliwa rasmi naye ni Bwana Trump.

Chini ya sheria za chama, wanachama 168 wa Kamati ya Taifa ya Republican, watapiga kura kumchagua mgombea mpya wa urais, kukiwa na uwezekano wa Mike Pence kuwa miongoni mwa wagombea watakaopigiwa kura.

Ikiwa Bwana Pence atachaguliwa, mgombea mpya wa urais atakuwa amechaguliwa.

Pence wears mask

Maelezo ya picha,

Makamu rais Pence atachukuwa majuku ya rais lakini hatakuwa mgombea wa chama cha Republican moja kwa moja

Sio chama cha Democrat wala Republican, hakuna ambacho kimewahi kubadilisha mgombea wake wa urais baada ya kuchaguliwa rasmi.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *