Viongozi wa Umoja wa Ulaya kuishinikiza Cyprus juu ya vikwazo vya Belarus,

October 1, 2020

 

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatazamiwa hivi leo kumaliza tafauti zao kuhusu suala la Belarus kwa kukabiliana na mkwamo mwengine na Uturuki, ambao umebainisha jinsi chombo hicho muhimu barani Ulaya kilivyo legelege kwenye kufikia maamuzi muhimu. 

Kwenye mkutano wa kilele wa siku mbili mjini Brussels unaoanza leo, viongozi hao wataikabili Cyprus, mmoja wa wanachama wadogo kabisa wa Umoja wa Ulaya, inayotuhumiwa kuzuwia kupitishwa kwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Belarus, kufuatia uchaguzi wa mwezi Agosti, ambao mataifa ya Magharibi na upinzani nchini humo wanasema uliibiwa. 

Wakati Uingereza na Canada zimesonga mbele kuichukulia hatua serikali ya Alexander Lukashenko na kuonesha uungaji mkono wao kwa wapigania demokrasia, mkwamo kwenye Umoja wa Ulaya umeathiri heshima ya chombo hicho kilimwengu. 

Kwa mujibu wa mkataba unaounda Umoja huo, uamuzi wowote unaohusu mahusiano na taifa jengine, lazima uridhiwe na kila mwanachama wa Umoja wa Ulaya. 

Cyprus inataka kwanza Umoja huo kuridhia vikwazo dhidi ya Uturuki kabla nayo kuridhia vya Belarus.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *