Viongozi wa Umoja wa Ulaya kufanya mkutano wa kilele kuhusu China mwezi ujao,

October 2, 2020

 

Viongozi wa Umoja wa Ulaya watafanya mkutano maalum wa kilele mwezi ujao mjini Berlin kujadili uhusiano usioeleweka wa Ulaya na China. 

Kulingana na ratiba ya Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya viongozi hao watakutana Novemba 16 bila ya China. 

Mkutano huo unakuja wakati ambapo Umoja wa Ulaya una wakati mgumu kuungana katika msimamo mmoja kuhusiana na China huku kukiwa na wasiwasi unaozidi kuongezeka kuhusiana na haki za binadamu nchini humo na biashara isiyo sawa. 

Viongozi 27 wa Umoja wa Ulaya wameonyesha wasiwasi mkubwa kuhusiana na ukiukaji wa haki za binadamu Hong Kong na dhidi ya jamii za wachache. 

Ujerumani ambayo hasa inashikilia urais wa muda wa Umoja wa Ulaya ina hamu sana ya kupatikana kwa makubaliano ya uwekezaji ya Umoja wa Ulaya na China kufikia mwishoni mwa mwaka.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *