Viongozi wa Kenya na Misri wajadiliana juu ya mzozo wa mto Nile,

October 8, 2020

Mkutano kati ya rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi na wa Kenya Uhuru Kenyatta umengazia majadiliano yaliokwama ya bwawa la Ethiopia, kulingana na maafisa wa Misri.

Viongozi hao wawili walikutana katika mji mkuu wa Cairo, Jumapili wakati rais Kenyatta anarejea nyumbani kutoka Ufaransa.

Taarifa kutoka kwa msemaji wa Misri inasema: “Mkutano huo uligusia maendeleo ya hivi karibu yenye maslahi ya mataifa hayo mawili, hasa yenye kuzingatia bwawa la Ethiopia, kama ilivyokubalika kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili wakati wa kipindi kijacho juu ya suala hili nyeti na muhimu”.

Kenya haikusema lolote kuhusu bwawa hilo zaidi ya kusema kuwa viongozi hao walijadiliana masuala yenye kugusa maslahi ya nchi hizo mbili, miongoni mwao amani ya eneo na usalama, biashara na namna Afrika inavyokabiliana na ugonjwa wa Covid-19″.

Bwawa la Ethiopia linalojengwa kutoka mto Nile linatarajiwa kutoa nguvu za umeme kwa raia milioni 65 wa Ethiopia.

Kwa kaisi kikubwa mno, Misri inategemea mto Nile kwa maji ya matumizi yake na hivi karibuni ilionya kwamba ujenzi wa bwawa hilo ni tishio kwa taifa lake.

Kenya ni mmoja wa waangalizi katika jopo la wapatanishi la Umoja wa Afrika kutatuza mgogoro unatokana na bwawa hilo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *