Viongozi wa dini watakiwa kuacha kupotosha watanzania kuhusu chanjo ya Corona,

August 4, 2021

Na Amiri Kilagalila,Njombe
Viongozi wa dini nchini wameshauriwa kuacha kuwapotosha wananchi kuhusu chanjo ya Corona kwani kufanya hivyo ni kuiingilia serikali katika kutimiza majukumu yake kwa wananchi inaowasimamia.
Kauli hiyo imetolewa na Mwinjilisti Asifiwe Mwasanyamba wa Kanisa la Kiinjili na Kirutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini usharika wa Melinze mkoani Njombe wakati wa ibada ya kuliombea taifa kwa siku nane ili kuondokana na ugonjwa wa Uviko 19.
“Kuna wengine wanapotosha kwa kusema chanjo hii ni mbaya,niwaulize ni nani aliyechoma hapa Tanzania akaona ni mbaya? Niseme tu serikali imewajibika na ingekuwa ya ajabu kama isingeonyesha kuwajibika na niwaaambie wakati wa vita hatuchagui silaha kwa hiyo lazima silaha yoyote tuitumie”Alisema  Asifiwe Mwasanyamba 
Mwasanyamba ameongeza kuwa “Tusisikilize propaganda kwasababu wasemaji wa serikali tunao,hawa wakisema juu ya taifa tuwasikilize na kwa kuwa kuna wengine wanapotosha juu Chanjo hawa tuwapuuze.Kwa hiyo sisi kama wainjilisti tunasema hivi mtu akitaka Chanjo achanjwe na asipotaka asichanjwe” 
Kwa upande wake kiongozi wa usharika huo mchungaji Eliad Siwelwe amesema kanisa hilo limekuwa likiwatahadharisha waumini wake kunawa mikono na kuvaa barakoa wanapokuwa kwenye ibada na hata wakiwa kwenye shughuli zingine ili kuendelea kupambana na virusi vya Corona.
“Juu ya chanjo tunawahimiza watu waweze kuchanja kwasababu kila mtu na imani yake lakini pia tumekuwa tukiwahamasisha waumini kuendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata njia zote za kujikinga na corona” Eliad Siwelwe Mchungaji kiongozi Usharika wa Melinze
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo akiwemo Amina Ilomo na Osward Mng’ong’o wanasema tahadhari dhidi ya Uviko 19 wanachukua ingawa mpaka sasa baadhi yao hawajaamua juu ya kupokea chanjo ya Uviko 19 na kuendelea kusisitizana kila mmoja afaute nafsi yake

 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *