Venezuela kushiriki jaribo la chanjo ya COVID-19 ya Urusi,

October 3, 2020

 

Venezuela imesema itashiriki katika awamu ya 3 ya majaribio ya chanjo ya Urusi ya Sputnik V dhidi ya virusi vya corona, kulingana na taarifa za jana za Makamu wa Rais Delcy Rodriguez. 

Waziri wa Afya wa Venezuela Carlos Alvarado amesema takriban raia 2,000 wa Venezuela watashiriki katika majaribio hayo ya chanjo ambayo yataanza mwezi huu, katika mji mkuu wa Caracas. 

Uhusiano wa Venezuela na Urusi umekuwa wa karibu zadi hivi karibuni, baada ya taifa hilo la Amerika Kusini kuwekewa vikwazo na Marekani, pamoja na mataifa mengine kadhaa kumuunga mkono kiongozi wa upinzani Juan Guido. Venezuela hadi hivi sasa imethibitisha maambukizi 76,000 ya virusi vya corona pamoja na vifo 635, ingawa inadaiwa idadi za kweli ni kubwa kuliko zilizotangazwa na serikali.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *