Vanessa Anogesha Penzi na Rotimi Kifuani Mwake

October 6, 2020

 

NI muendelezo wa matukio ya mahusiano ambayo yanafuatiliwa na watu wengi hapa nchini Tanzania kati ya msanii Vanessa Mdee na mpenzi wake Rotimi wa Nigeria na Marekani baada ya kuchorana tattoo kwenye miili yao.

 

Video ambazo zimetawala kwenye mitandao ya kijamii zimewaonyesha kila mmoja kumchora tattoo mwenzake ikiwa kama ni ishara ya upendo, urembo na kumbukumbu kwenye mahusiano yao.

 

Rotimi amesema ana michoro mingi kwenye mwili wake ikiwemo ya picha ya Yesu, ‘Ego’, Simba na sehemu ya peponi, pia akaongeza kusema ana tattoo yenye jina la Vanessa Mdee mkononi mwake.

 

Aidha kwa upande wa Vanessa Mdee, yeye akaonyesha tattoo yenye jina la Rotimi ambayo ameichora maeneo ya kifuani mwake.

 

Siku kadhaa zijazo wawili hao wanatarajia kutimiza mwaka mmoja tangu walipoanzisha mahusiano yao mwezi Oktoba 2019.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *