UWT yawataka wanawake kumpigia kur Dkt. Hussein Mwinyi, on September 18, 2020 at 1:00 pm

September 18, 2020

 Na Thabit Madai,Zanzibar.JUMUIYA ya  Wanawake (UWT) Mkoa wa Kaskazini Unguja, imewataka wanawake wote mkoani humo kuhakikisha kila mwanamke  anasaka kura za ushindi kwa mgombea Urais wa CCM, Dk. Hussein Ali Mwinyi  ,ashinde   na kuwaacha midomo wazi wagombea  wa upinzanHayo yameelezwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja, Maryam Muharam Shomari,  huko Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja.Mwenyekiti huyo amesema kwamba wanawake wana nguvu kubwa katika jamii hivyo ni wajbu wao kuhakikisha wagombea wa CCM Ndani ya mkoa huo wanashinda kwa kishindo na kuwaacha midomo wazi wagombea wa upinzani.Amesema wagombea wa chama cha Mapinduzi CCM wanakila sifa za kuweza kuongoza kutoka na mchakato wa upatikaji wao hivyo kila mwananchama wa CCM anapaswa kuhakikisha wagombea hao wanapata ushindi wa kishindo.Maryam amesema  CCM  kimeonyesha uimara na nguvu zake utaothibitika Oktoba 28, mwaka huu pale mgombea wa CCM atakapoibuka kidedea na kuingia Ikulu.Ameeleza kuwa  CCM ni chama  kilichotokana na ASP kwa upande wa Zanzibar  bado kina nguvu kubwa kisiasa, na kinaungwa mkono na wananchi kwani  kimekuwa kinatimiza ahadi zake sera na kusimamia ipasavyo misingi ya amani , umoja na maendeleo.Ameongeza kueleza kwamba Upinzani ulioanzishwa  mwaka 1992 hautashindana na nguvu za kisiasa zilizowekezwa tokea mwaka 1957.CCM kitaendelea kuaminiwa kwa msimamo yake imara,  sera za mshikamano ,amani na umoja wakati upinzani ukijoandaa kushabilia machafuko, kutaka zifanyike ghasia mitaani na kuitishwa maandamano.,

 Na Thabit Madai,Zanzibar.

JUMUIYA ya  Wanawake (UWT) Mkoa wa Kaskazini Unguja, imewataka wanawake wote mkoani humo kuhakikisha kila mwanamke  anasaka kura za ushindi kwa mgombea Urais wa CCM, Dk. Hussein Ali Mwinyi  ,ashinde   na kuwaacha midomo wazi wagombea  wa upinzan

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja, Maryam Muharam Shomari,  huko Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja.

Mwenyekiti huyo amesema kwamba wanawake wana nguvu kubwa katika jamii hivyo ni wajbu wao kuhakikisha wagombea wa CCM Ndani ya mkoa huo wanashinda kwa kishindo na kuwaacha midomo wazi wagombea wa upinzani.

Amesema wagombea wa chama cha Mapinduzi CCM wanakila sifa za kuweza kuongoza kutoka na mchakato wa upatikaji wao hivyo kila mwananchama wa CCM anapaswa kuhakikisha wagombea hao wanapata ushindi wa kishindo.

Maryam amesema  CCM  kimeonyesha uimara na nguvu zake utaothibitika Oktoba 28, mwaka huu pale mgombea wa CCM atakapoibuka kidedea na kuingia Ikulu.

Ameeleza kuwa  CCM ni chama  kilichotokana na ASP kwa upande wa Zanzibar  bado kina nguvu kubwa kisiasa, na kinaungwa mkono na wananchi kwani  kimekuwa kinatimiza ahadi zake sera na kusimamia ipasavyo misingi ya amani , umoja na maendeleo.

Ameongeza kueleza kwamba Upinzani ulioanzishwa  mwaka 1992 hautashindana na nguvu za kisiasa zilizowekezwa tokea mwaka 1957.CCM kitaendelea kuaminiwa kwa msimamo yake imara,  sera za mshikamano ,amani na umoja wakati upinzani ukijoandaa kushabilia machafuko, kutaka zifanyike ghasia mitaani na kuitishwa maandamano.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *