Utawala wa kijeshi Myanmar wamfungulia mashtaka ya rushwa Suu Kyi,

June 10, 2021

Utawala wa kijeshi nchini Myanmar umemfunguliwa kiongozi wa kiraia aliepinduliwa Aung San Suu Kyi, mashtaka ya rushwa, kuhusiana na madai kwamba alikubali malipo haramu ya dhahabu na zaidi ya dola nusu milioni fedha taslimu.

Mashtaka hayo ya karibuni zaidi yanahusiana na madai ya waziri kiongozi wa zamani wa mkoa wa Yangon, kwamba Suu Kyi alipokea kinyume cha sheria pesa taslimu dola laki sita kutoka kwake, pamoja na kilo karibu 11 za dhahabu. 

Kwa mujibu wa gazeti la serikali la Global New Light of Myanmar, tume ya kupambana na rushwa imepata ushahidi kwamba Suu Kyi alikuwa ametenda vitendo vya rushwa kwa kutumia cheo chake. 

Pia anashtumiwa kwa kutumia vibaya madaraka yake wakati alipokodisha maeneo mawili ya ardhi kwa ajili ya wakfu wake wa hisani. 

Lakini wakili wake Khin Maung Zaw, ameyatupilia mbali mashtaka hayo kuwa ya kipuuzi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *