Urusi, China zahimiza kurejeshwa utulivu Kyrgyzstan,

October 7, 2020

 

Rais Vladimir Puti wa Urusi amesema nchi yake inatiwa wasiwasi na mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Kyrgyzstan, na kutoa wito wa kurejeshwa kwa utulivu haraka iwezekanavyo. 

Nchi hiyo ya Asia ya kati ambako Urusi ina kituo cha jeshi lake la anga, imeangukia katika vurugu tangu wanaharakati wa upinzani walipovamia ofisi za serikali Jumanne wiki hii, na kumlazimisha waziri mkuu kujiuzulu, na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa bunge. 

Putin amesema wanayo mawasiliano na wadau wote kwenye mzozo huo. China mbayo pia inapakana na Kyrgyzstan imesema hali inayojiri katika taifa hilo ni ya wasiwasi mkubwa, na kuhimiza kurejeshwa kwa mazingira ya amani. 

Baadhi ya biashara za makampuni ya kigeni nchini Kyrgyzstan zimeshambuliwa na makundi ambayo bado hayajatambuliwa, na kuzidisha hali ya mashaka na hofu kuwa nchi hiyo inaweza kutumbukia katika ghasia.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *