“Urais Nitashinda Tena Kwa Kura nyingi”- Magufuli Aweka Wazi

September 18, 2020

Mgombea Urais kupitia CCM Dkt John Magufuli amewahakikishia wananchi wa Kibondo mkoani Kigoma kuwa katika uchaguzi mkuu ujao atashinda kwa kura nyingi kwani Watanzania wa maeneo yote wanamtaka yeye.Dkt Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 17, 2020, wakati akiendelea na mikutano yake ya kampeni katika maeneo mbalimbali huku akisisitiza wananchi kumchagulia madiwani na wabunge kutoka chama hicho.”Nitasikitika sana kama hamtanichagulia wabunge na madiwani wa CCM kwa sababbu mimi Urais nitashinda tu tena kwa kura nyingi sana na ninataka niwahakikishie kwa sababu watanzania maeneo yote wanamtaka Magufuli”, amesema Dkt Magufuli.Aidha Magufuli akatoa rai kwa wana CCM wale ambao hawakuchaguliwa kuwani nafasi katika uchaguzi mkuu ujao, “Naomba wana CCM wenzangu mliokosa nafasi msinunue, kuchaguliwa pia ni mipango ya Mungu, yule mbunge wa Busanda amegombea mara nne, miaka mitano iliyopita nikamteua kuwa DC mwaka huu ndiye anayegombea pale, hata mliogombea mwaka huu msikate tamaa”.,

Mgombea Urais kupitia CCM Dkt John Magufuli amewahakikishia wananchi wa Kibondo mkoani Kigoma kuwa katika uchaguzi mkuu ujao atashinda kwa kura nyingi kwani Watanzania wa maeneo yote wanamtaka yeye.

Dkt Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 17, 2020, wakati akiendelea na mikutano yake ya kampeni katika maeneo mbalimbali huku akisisitiza wananchi kumchagulia madiwani na wabunge kutoka chama hicho.

“Nitasikitika sana kama hamtanichagulia wabunge na madiwani wa CCM kwa sababbu mimi Urais nitashinda tu tena kwa kura nyingi sana na ninataka niwahakikishie kwa sababu watanzania maeneo yote wanamtaka Magufuli”, amesema Dkt Magufuli.

Aidha Magufuli akatoa rai kwa wana CCM wale ambao hawakuchaguliwa kuwani nafasi katika uchaguzi mkuu ujao, “Naomba wana CCM wenzangu mliokosa nafasi msinunue, kuchaguliwa pia ni mipango ya Mungu, yule mbunge wa Busanda amegombea mara nne, miaka mitano iliyopita nikamteua kuwa DC mwaka huu ndiye anayegombea pale, hata mliogombea mwaka huu msikate tamaa”.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *