Upinzani Belarus waanzisha chama kipya cha kutafuta mageuzi, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 1, 2020 at 10:00 am

September 1, 2020

Mwanasiasa wa upinzani wa Belarus Maria Kolesnikova ametangaza kuanzisha chama kipya ambacho kitatafuta mageuzi ya kisiasa, kijamii na kiuchumi nchini humo. Kolesnikova mwenye umri wa miaka 38, amesema chama hicho kipya kinachoitwa Vmeste, kumaanisha “pamoja”, kinalenga kutoa jukwaa kwa wale wanaotafuta mabadiliko. Kolesnikova ni mkuu wa zamani wa kampeni za Viktor Babariko, mgombea wa upinzani aliyefungwa jela kabla ya uchaguzi wa Agosti 9. Amekuwa mmoja wa vigogo maarufu katika vuguvugu la dhidi ya kiongozi wa nchi hiyo anayepingwa Alexander Lukashenko.Lukashenko, mwenye umri wa miaka 66, ameiongoza jamhuri hiyo ya uliokuwa muungano wa Kisovieti katika Ulaya mashariki kwa zaidi ya robo karne, kwa kuukandamiza upinzani.,

Mwanasiasa wa upinzani wa Belarus Maria Kolesnikova ametangaza kuanzisha chama kipya ambacho kitatafuta mageuzi ya kisiasa, kijamii na kiuchumi nchini humo. 

Kolesnikova mwenye umri wa miaka 38, amesema chama hicho kipya kinachoitwa Vmeste, kumaanisha “pamoja”, kinalenga kutoa jukwaa kwa wale wanaotafuta mabadiliko.

 Kolesnikova ni mkuu wa zamani wa kampeni za Viktor Babariko, mgombea wa upinzani aliyefungwa jela kabla ya uchaguzi wa Agosti 9. 

Amekuwa mmoja wa vigogo maarufu katika vuguvugu la dhidi ya kiongozi wa nchi hiyo anayepingwa Alexander Lukashenko.

Lukashenko, mwenye umri wa miaka 66, ameiongoza jamhuri hiyo ya uliokuwa muungano wa Kisovieti katika Ulaya mashariki kwa zaidi ya robo karne, kwa kuukandamiza upinzani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *