UN:Vikosi vya Maduro vilitekeleza uhalifu wa kibinadamu

September 16, 2020

Wachunguzi hao wa umoja wa mataifa walisema kuwa, kulikuwa na sababu za msingi kuamini kwamba Rais Nicolas Maduro na mawaziri wake wa mambo ya ndani na ulinzi waliamuru au wamechangia uhalifu ulioandikwa katika ripoti hiyo ili wawanyamazishe wapinzani.

Aidha wachunguzi hao wameongeza kusema kuwa, utekelezaji wa mauaji mengi haramu ulifanywa na mawakala wa serikali na hawajafunguliwa mashitaka nchini Venezuela ambapo utawala wa sheria na taasisi za kidemokrasia zimeminywa.

Ujumbe wa kutafuta ukweli wa Umoja wa mataifa ulisema kuwa sheria nyingine za kitaifa na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu (ICC), ambayo ilifungua uchunguzi wa awali nchini Venezuela mnamo mwaka 2018, inapaswa fikiria mashitaka. Ingeshirikisha hifadhidata yake iliyo na majina ya maafisa waliotambuliwa na waathiriwa.

“Ujumbe ulibaini sababu nzuri za kuamaini kwamba mamlaka za venezuela na vikosi vya usalama tangu mwaka 2014 vilipanga na kutekeleza ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu baadhi yake ni pamoja na mauaji ya kiholela na mateso ya kimfumo, kiasi cha uhalifu dhidi ya ubinadamu,”Mwenyekiti wa jopo Marta Valinas alisema katika taarifa hiyo.

Hakukuwa na jibu la mara moja kutoka katika serikali ya mrengo wa kushoto ya Maduro kwa ripoti hiyo kwa kuzingatia mahojiano zaidi ya 270 na wathiriwa, mashahidi, maafisa wa zamani na mawakili na nyaraka za siri.

Chanzo/RTRE

 

Source link

,Wachunguzi hao wa umoja wa mataifa walisema kuwa, kulikuwa na sababu za msingi kuamini kwamba Rais Nicolas Maduro na mawaziri…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *