UN yaelezea wasiwasi kuhusu matukio ya karibuni ya mzozo wa Libya, noreply@blogger.com (Muungwana Blog), on August 29, 2020 at 6:00 pm

August 29, 2020

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi kuhusu kile ulichokiita “mabadiliko ya ghafla ya matukio” katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya, baada ya mvutano wa madaraka kati ya viongozi wa serikali ya Tripoli kutokea kufuatia maandamano ya kupinga ufisadi.Ujumbe wa msaada wa Umoja wa Mataifa nchini Libya umesema Libya inashuhudia mabadiliko ya ghafla ya matukio ambayo yanasisitiza haja ya dharura ya kurejea katika mchakato kamili wa kisiasa na unaozijumuisha pande zote.Kiongozi wa serikali ya Libya inayotambulika kimataifa Fayez al Sarraj amemsimamisha kazi waziri wake wa mambo ya ndani mwenye nguvu Fathi Bashagha, akisema kuwa atafanyiwa uchunguzi wa namna alivyoyashughulikia maandamano na ukandamizaji dhidi ya waandamanaji.Hatua hiyo inakwenda sanjari na ripoti za kuongezeka mvutano kati ya Sarraj na waziri huyo, ambaye ni kiongozi mwenye ushawishi mkubwa kutokea mji wa bandari na ngome ya kijeshi ya Misrata.,

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi kuhusu kile ulichokiita “mabadiliko ya ghafla ya matukio” katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya, baada ya mvutano wa madaraka kati ya viongozi wa serikali ya Tripoli kutokea kufuatia maandamano ya kupinga ufisadi.

Ujumbe wa msaada wa Umoja wa Mataifa nchini Libya umesema Libya inashuhudia mabadiliko ya ghafla ya matukio ambayo yanasisitiza haja ya dharura ya kurejea katika mchakato kamili wa kisiasa na unaozijumuisha pande zote.

Kiongozi wa serikali ya Libya inayotambulika kimataifa Fayez al Sarraj amemsimamisha kazi waziri wake wa mambo ya ndani mwenye nguvu Fathi Bashagha, akisema kuwa atafanyiwa uchunguzi wa namna alivyoyashughulikia maandamano na ukandamizaji dhidi ya waandamanaji.

Hatua hiyo inakwenda sanjari na ripoti za kuongezeka mvutano kati ya Sarraj na waziri huyo, ambaye ni kiongozi mwenye ushawishi mkubwa kutokea mji wa bandari na ngome ya kijeshi ya Misrata.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *