UN: Janga la virusi vya corona linatishia mamilioni ya watoto, on September 9, 2020 at 10:00 am

September 9, 2020

 Kuvurugika kwa huduma za afya kutokana na janga la virusi vya corona kunaweka maisha ya mamilioni ya watu katika hatari duniani kote, Umoja wa Mataifa umesema leo, ukionya kuwa COVID-19 inabadilisha mafanikio yaliyopatikana miongo kadhaa iliyopita katika kupunguza vifo vya watoto. Miaka 30 iliyopita imeshuhudia hatua kubwa zilizopigwa kuzuwia ama kutibu sababu za vifo vya watoto ikiwa ni pamoja na vifo vya mapema na kichomi. Makadirio mapya ya vifo yaliyochapishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudimia watoto UNICEF, shirika la afya ulimwenguni na kundi la benki kuu ya dunia imegundua kuwa mwaka 2019 ulishuhudia idadi ya chini kabisa ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano duniani. Mwaka jana watoto milioni 5.2 walifariki kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika, ikilinganishwa na watoto milioni 12.5 mwaka 1990.,

 

Kuvurugika kwa huduma za afya kutokana na janga la virusi vya corona kunaweka maisha ya mamilioni ya watu katika hatari duniani kote, Umoja wa Mataifa umesema leo, ukionya kuwa COVID-19 inabadilisha mafanikio yaliyopatikana miongo kadhaa iliyopita katika kupunguza vifo vya watoto.

 Miaka 30 iliyopita imeshuhudia hatua kubwa zilizopigwa kuzuwia ama kutibu sababu za vifo vya watoto ikiwa ni pamoja na vifo vya mapema na kichomi. 

Makadirio mapya ya vifo yaliyochapishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudimia watoto UNICEF, shirika la afya ulimwenguni na kundi la benki kuu ya dunia imegundua kuwa mwaka 2019 ulishuhudia idadi ya chini kabisa ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano duniani. 

Mwaka jana watoto milioni 5.2 walifariki kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika, ikilinganishwa na watoto milioni 12.5 mwaka 1990.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *