Umoja wa Ulaya waionya Uingereza kuhusu Brexit, on September 7, 2020 at 5:00 pm

September 7, 2020

Kiongozi wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen ameionya Uingereza kwamba ina wajibu wa kuheshimu makubaliano ya kuondoka Umoja wa Ulaya, Brexit, ambayo yanapaswa kuweka misingi kuhusu uhusiano wa baadaye.Rais huyo wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya amesema anaiamini serikali ya Uingereza katika utekelezaji wa makubaliano hayo ya Brexit na wajibu wake chini ya sheria ya kimataifa na masharti yaliyopo kuhusu uhusiano wa baadaye.Halmashauri ya Umoja wa Ulaya pia imesema kwamba iko tayari kufikia haraka makubaliano na Uingereza kuhusu uhusiano wa baadaye wa kiuchumi na kibiashara lakini pia umoja huo umesisitiza kwamba makubaliano hayo yatapaswa kuhakikisha haki na ushindani huru.,

Kiongozi wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen ameionya Uingereza kwamba ina wajibu wa kuheshimu makubaliano ya kuondoka Umoja wa Ulaya, Brexit, ambayo yanapaswa kuweka misingi kuhusu uhusiano wa baadaye.

Rais huyo wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya amesema anaiamini serikali ya Uingereza katika utekelezaji wa makubaliano hayo ya Brexit na wajibu wake chini ya sheria ya kimataifa na masharti yaliyopo kuhusu uhusiano wa baadaye.

Halmashauri ya Umoja wa Ulaya pia imesema kwamba iko tayari kufikia haraka makubaliano na Uingereza kuhusu uhusiano wa baadaye wa kiuchumi na kibiashara lakini pia umoja huo umesisitiza kwamba makubaliano hayo yatapaswa kuhakikisha haki na ushindani huru.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *