Umoja wa Mataifa wasema Rais wa Venezuela Maduro anahusika na uhalifu dhidi ya binadamu, on September 16, 2020 at 5:00 pm

September 16, 2020

 Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamesema leo kuwa wanamhusisha Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo uhalifu dhidi ya binadamu. Katika ripoti ya kurasa 411 Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kutafuta ushahidi Venezuela umesema umepata ushahidi wa uhalifu uliokuwa na lengo la kuukandamiza upinzani, ikiwemo mpango maalum wa kuwafunga jela, kuwapoteza, kuwatesa, kuwadhalilisha kingono na kuwauwa. Kulingana na ripoti hiyo, uhalifu huo umekuwa ukifanywa tangu mwaka 2014. Ripoti hiyo vile vile inasema demokrasia na sheria hazizingatiwi Venezuela katika miaka ya hivi karibuni kwani bunge la nchi hiyo lililokuwa na wabunge wengi wa upinzani lilifungwa, serikali ikapanua mamlaka yake na majaji wakawa wanakabiliwa na shinikizo kubwa.,

 

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamesema leo kuwa wanamhusisha Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo uhalifu dhidi ya binadamu. 

Katika ripoti ya kurasa 411 Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kutafuta ushahidi Venezuela umesema umepata ushahidi wa uhalifu uliokuwa na lengo la kuukandamiza upinzani, ikiwemo mpango maalum wa kuwafunga jela, kuwapoteza, kuwatesa, kuwadhalilisha kingono na kuwauwa. 

Kulingana na ripoti hiyo, uhalifu huo umekuwa ukifanywa tangu mwaka 2014. 

Ripoti hiyo vile vile inasema demokrasia na sheria hazizingatiwi Venezuela katika miaka ya hivi karibuni kwani bunge la nchi hiyo lililokuwa na wabunge wengi wa upinzani lilifungwa, serikali ikapanua mamlaka yake na majaji wakawa wanakabiliwa na shinikizo kubwa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *