Umoja wa Mataifa wasema mauaji ya halaiki Colombia yanaongezeka,

October 2, 2020

 Umoja wa Mataifa unasema Colombia imesajili karibu mauaji 42 ya halaiki tangu mwanzoni mwa mwaka 2020. 

Umoja huo unasema hii ni idadi kubwa zaidi kwa mwaka tangu kutiwa saini kwa makubaliano ya mwaka 2016 na waliokuwa waasi wa FARC. 

Umoja wa Mataifa unasema katibu wake mkuu Antonio Guterres ana wasiwasi kuhusiana na ongezeko la mauaji yanayoendelea katika maeneo kadhaa katika nchi hiyo ya kusini mwa Amerika katika miezi michache iliyopita. 

Kulingana na Umoja wa mataifa, mauaji ya halaiki ni kuuwawa kwa watu watatu au zaidi kwa wakati mmoja. Umoja huo vile vile unasema kuwa visa 13 vya mauaji ya halaiki vinachunguzwa. 

Tume ya amani ya Umoja wa mataifa ilisarekodi mauaji 36 ya halaiki nchini Colombia mwaka 2019, mwaka 2018 ikasajili mauaji 29 na mwaka 2017 ikasajili mauaji 11 ya aina hiyo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *