Ujerumani yasema Alexei Navalny alitiliwa sumu ya Novichok, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 3, 2020 at 8:00 am

September 3, 2020

Kuna ushahidi uliodhahiri kuwa mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny alipewa sumu ya Novichok inayoathiri neva, Ujerumani imesema.Chansela Angela Merkel alisema kuwa mwanasiasa huyo alinusurika kuuawa na dunia itatafuta majibu kutoka kwa Urusi.Bwana Navalny alisafirishwa Ujerumani baada ya kuanza kuugua akiwa ndani ya ndege huko Siberia mwezi uliopita na bado hadi sasa amepoteza fahamu.Timu yake inasema alitiliwa simu kwa maagizo ya Rais Vladimir Putin. Hata hivyo Urusi imekanusha madai hayo.Msemaji wa Urusi aliitaka Ujerumani kuishirikisha taarifa zake zote huku msemaji wa wizara ya mambo ya nje Maria Zakharova akilalamika kwamba madai ya Novichok hayakuambatinishwa na ushahidi wowote. “Ukweli uko wapi, ni mchakato gani uliotumika, yaani hata mutoe taarifa?” alisema.Sumu inayoathiri neva ya Novichok ilitumiwa kwa aliyekuwa jasusi wa Urusi Sergei Skripal na binti yake wakiwa Uingereza mwaka 2018. Ingawa wao walinusurika, mwanamke mwingireza alifariki baadae akiwa hospitalini. Uingereza ilishutumu jeshi la Uingereza kwa kutekeleza shambulio hilo.Waziri Mkuu Boris Johnson alishutumu shambulio la hivi karibu na kulitaja kama aibu. Serikali ya Urusi sasa ni lazima ielezee nini kilichotokea kwa Bwana Navalny – tutashirikiana na washirika wa kimataifa kuhakikisha haki inatendeka” aliandika kupitia ujumbe wa Twitter.Baada ya serikali ya Ujerumani kutoka matokeo ya vipimo vya kubainisha ikiwa mwanasiasa huo alitiwa sumu vilivyofanyika katika maabara ya kijeshi ya Chansela Merkel alisema kwamba “sasa kuna maswali nyeti ambayo ni serikali ya Urusi tu inaweza na ni lazima ijibu”.”Baadhi walijaribu kumnyamazisha Bwana Navalny na kwa niaba ya serikali yote ya Ujerumani, nashutumu hilo kwa nguvu yote.”Chansela Merkel alisema washrika wa Ujerumani Nato na EU wamefahamishwa matokeo ya uchunguzi huo na wataamua hatua ya pamoja stahiki ya kuchukua kulingana na jinsi Urusi itakavyojibu.Mke wa Navalny, Yulia Navalnaya na balozi wa Ujrusi nchini Ujerumani pia watafahamishwa kuhusu matoke ohayo serikali ya Ujerumani imesema.Muungano wa Ulaya imetaka uchunguzi wa wazi kufanywa na serikali ya Urusi. “Walihusika lazima wawajibishwe,” taarifa hiyo imesema.Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg pia alitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi kupitia ujumbe aliandika kwenye mtandao wa Twitter, huku Baraza la Taifa la Usalama Marekani, likisema tukio hilo linaloshukiwa kuhusisha sumu ni aibu na halikubaliki kabisa”.”Tutashirikiana na washirika wengine na jumuiya ya kimataifa kuhakikisha waliotekeleza kitendo hicho huko Urusi wanawajibishwa punde tu ushahidi utakapopatikana na kusitisha ufadhili wa vitendo vyao vya kiovu,” msemaji wa Baraza la Usalama la Marekani amesema.,

Kuna ushahidi uliodhahiri kuwa mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny alipewa sumu ya Novichok inayoathiri neva, Ujerumani imesema.

Chansela Angela Merkel alisema kuwa mwanasiasa huyo alinusurika kuuawa na dunia itatafuta majibu kutoka kwa Urusi.

Bwana Navalny alisafirishwa Ujerumani baada ya kuanza kuugua akiwa ndani ya ndege huko Siberia mwezi uliopita na bado hadi sasa amepoteza fahamu.

Timu yake inasema alitiliwa simu kwa maagizo ya Rais Vladimir Putin. Hata hivyo Urusi imekanusha madai hayo.

Msemaji wa Urusi aliitaka Ujerumani kuishirikisha taarifa zake zote huku msemaji wa wizara ya mambo ya nje Maria Zakharova akilalamika kwamba madai ya Novichok hayakuambatinishwa na ushahidi wowote. “Ukweli uko wapi, ni mchakato gani uliotumika, yaani hata mutoe taarifa?” alisema.

Sumu inayoathiri neva ya Novichok ilitumiwa kwa aliyekuwa jasusi wa Urusi Sergei Skripal na binti yake wakiwa Uingereza mwaka 2018. Ingawa wao walinusurika, mwanamke mwingireza alifariki baadae akiwa hospitalini. Uingereza ilishutumu jeshi la Uingereza kwa kutekeleza shambulio hilo.

Waziri Mkuu Boris Johnson alishutumu shambulio la hivi karibu na kulitaja kama aibu. Serikali ya Urusi sasa ni lazima ielezee nini kilichotokea kwa Bwana Navalny – tutashirikiana na washirika wa kimataifa kuhakikisha haki inatendeka” aliandika kupitia ujumbe wa Twitter.

Baada ya serikali ya Ujerumani kutoka matokeo ya vipimo vya kubainisha ikiwa mwanasiasa huo alitiwa sumu vilivyofanyika katika maabara ya kijeshi ya Chansela Merkel alisema kwamba “sasa kuna maswali nyeti ambayo ni serikali ya Urusi tu inaweza na ni lazima ijibu”.

“Baadhi walijaribu kumnyamazisha Bwana Navalny na kwa niaba ya serikali yote ya Ujerumani, nashutumu hilo kwa nguvu yote.”

Chansela Merkel alisema washrika wa Ujerumani Nato na EU wamefahamishwa matokeo ya uchunguzi huo na wataamua hatua ya pamoja stahiki ya kuchukua kulingana na jinsi Urusi itakavyojibu.

Mke wa Navalny, Yulia Navalnaya na balozi wa Ujrusi nchini Ujerumani pia watafahamishwa kuhusu matoke ohayo serikali ya Ujerumani imesema.

Muungano wa Ulaya imetaka uchunguzi wa wazi kufanywa na serikali ya Urusi. “Walihusika lazima wawajibishwe,” taarifa hiyo imesema.

Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg pia alitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi kupitia ujumbe aliandika kwenye mtandao wa Twitter, huku Baraza la Taifa la Usalama Marekani, likisema tukio hilo linaloshukiwa kuhusisha sumu ni aibu na halikubaliki kabisa”.

“Tutashirikiana na washirika wengine na jumuiya ya kimataifa kuhakikisha waliotekeleza kitendo hicho huko Urusi wanawajibishwa punde tu ushahidi utakapopatikana na kusitisha ufadhili wa vitendo vyao vya kiovu,” msemaji wa Baraza la Usalama la Marekani amesema.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *