Ujerumani yaongeza shinikizo kwa Urusi kuhusu Navalny, on September 6, 2020 at 5:00 pm

September 6, 2020

Ujerumani leo imeongeza shinikizo dhidi ya Urusi kuhusiana na tukio la kupewa sumu kwa kiongozi wa upinzani nchini humo Alexei Navalny na kuonya kuwa kukosekana kwa ushirikiano kutoka kwa Urusi katika uchunguzi kuhusu tukio hilo huenda ”ukailazimu” Ujerumani kutafakari upya kuhusu mradi wa bomba la gesi la Nord Stream 2 kati yake na Urusi. Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas, ameliambia gazeti la kila siku la Ujerumani Bild kwamba anatumaini Urusi haitawalazimisha kubadili msimamo wao kuhusu bomba hilo la gesi linalojengwa chini ya bahari ya Baltic.Maas ameongeza kwamba iwapo hakutakuwa na ushirikiano kutoka kwa Urusi katika siku chache zijazo, itawabidi kushauriana na washirika wao.Hata hivyo Maas pia alikiri kwamba kusimamisha ujenzi wa bomba hilo la gesi linalokaribia kukamilika, kutaiathiri Ujerumani na kampuni za Ulaya.Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alitaja tukio la kupewa sumu kwa Navalny kuwa jaribio la mauaji yaliyolenga kumnyamazisha mkosoaji mkubwa wa Putin na kutoa wito wa uchunguzi kamili.,

Ujerumani leo imeongeza shinikizo dhidi ya Urusi kuhusiana na tukio la kupewa sumu kwa kiongozi wa upinzani nchini humo Alexei Navalny na kuonya kuwa kukosekana kwa ushirikiano kutoka kwa Urusi katika uchunguzi kuhusu tukio hilo huenda ”ukailazimu” Ujerumani kutafakari upya kuhusu mradi wa bomba la gesi la Nord Stream 2 kati yake na Urusi.

 Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas, ameliambia gazeti la kila siku la Ujerumani Bild kwamba anatumaini Urusi haitawalazimisha kubadili msimamo wao kuhusu bomba hilo la gesi linalojengwa chini ya bahari ya Baltic.

Maas ameongeza kwamba iwapo hakutakuwa na ushirikiano kutoka kwa Urusi katika siku chache zijazo, itawabidi kushauriana na washirika wao.

Hata hivyo Maas pia alikiri kwamba kusimamisha ujenzi wa bomba hilo la gesi linalokaribia kukamilika, kutaiathiri Ujerumani na kampuni za Ulaya.Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alitaja tukio la kupewa sumu kwa Navalny kuwa jaribio la mauaji yaliyolenga kumnyamazisha mkosoaji mkubwa wa Putin na kutoa wito wa uchunguzi kamili.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *